Ticker

6/recent/ticker-posts

ZAIDI YA TANI SABA YA BIDHAA ZILIZOMALIZA MUDA WAKE ZIMETEKETEZWA NA SHIRIKA LA VIWANGO TANZANIA ( TBS ) JIJINI MWANZA.


 

Akizungumza Mara baada ya zoezi hilo la uteketezaji wa bidhaa hizo Afisa udhibiti ubora mwandamizi kutoka ofisi ya Kanda ya ziwa TBS Nuru Edgar Mwasulama amesema hayo ni matokeo ambayo ofisi ya Kanda ya ziwa imekuwa ikifanya kwa mwaka wa fedha wa 2023/ 2024 ambapo bidhaa zisiso na ubora zimekuwa zikiondolewa kwenye masoko na bidhaa ambazo zimepigwa marufuku Kama vile vipodozi vyenye viambata vya sumu na vilainishi vya magari D.O.T 3 ambavyo navyo vimepigwa marufuku kwakuwa havina ubora .

 

 " Uwa tuna shejo oparesheni mbali mbali kwenye mfumo wetu wa udhibiti tunaita ni spesho uparesheni kontro ambazo zimegawanyika katika makundi mbali mbali, Kuna vipodozi vimeondolewa katika Soko, vilainishi ambavyo vimepigwa marufuku vya magari na maziwa ya watoto wachanga ambayo ayajasajiliwa ."

 


 Aidha Edgar ameongeza kuwa zoezi Hilo ni endelevu na Mazoezi haya uwa yanafanyika kwa kushitukiza katika masoko yetu ya Kanda ya ziwa Na Nchi nzima kwa ujumla kwa Sababu shirika lipo Nchi nzima na wanaofisi ya Kanda Katika mikoa yote na nishughuli za udhibiti na nimatokeo ya mikoa yote.

 

Mbali na hayo Edgar ameongeza kuwa kazi yao Kama TBS sio kukamata Na kuteketeza bali wanajenga uwelewa kwa wadau mbali mbali Na kutoa Elimu Na Moja ya vipodozi tulivyoteketeza ni matokeo ya wateje kutoa taarifa.

 

Kwa pande wake Afisa udhibiti ubora TBS Kanda ya ziwa Deus Mlenga ametoa wito kwa wananchi wote wa Kanda ya ziwa na Tanzania kwa ujumla wanapoona bidhaa zozote zile ambazo zimeisha muda wa matumizi na bidhaa ambazo Zina viambata vya sumu waweze kutoa taarifa kwa Wakati .


 



 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments