ZINAHITAJIKA JUHUDI NA NGUVU YA PAMOJA KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO YA UHAMIAJI - CHIEF CHARUMBIRA

Bengazi

Rais wa  Bunge la Afrika Chief Fortune Charumbira amesema Bunge hilo lina wajibu mkubwa wa  kukuza na kuimarisha misingi ya haki za binaadamu,  demokrasia  na utawala bora , uwazi  pamoja na uwajibikaji  katika Nchi wanachama barani Afrika,hasa katika hatua za kushughulikia uhamiaji  

Ameyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa kwenye  Mkutano wa Kimataifa wa Uhamiaji wa Euro-Afrika Mjini Benghazi Nchini Libya ambapo ametaka kuweka umadhubuti kuhakikisha kunakuwa na uhamiaji wenye manufaa kwa pande zote kupitia sera na mipango baina ya maeneo husika

Chief Charumbira ameeleza kuwa pamoja na mambo mengine Mkutano huo  umelenga kujadili na kuangalia namna bora ya kutatua changamoto ya uhamiaji kuvuka na kuingia Italia  na Malta kupitia Libya, ili kuondokana na athari za uhamiaji haramu,hivyo kukuza zaidi Amani,usalama, utulivu,  ushirikiano na maendeleo barani Afrika

Ameeleza zaidi kuwa hatua hiyo imelenga kukabiliana uhamiaji haramu ambao umekuwa ukisababisha athari kwa raia ambao wanafanya biashara halali

“kwa kuzingatia ukweli kwamba,  hivi karibuni, Libya ilikuwa sehemu kuu ya kuondoka  wahamiaji kuelekea  bara la Ulaya,na kwamba tangu wakati huo Tunisia imeipiku Libya kwa zaidi ya  asilimia 62% ya watu zaidi ya 150 000 waliovuka Katika eneo la  Mediterranean kwa kutumia usafiri wa  boti mwaka  2023”

“Njia ya kati ya mediterania (njia ya kutoka Algeria, misri, Libya na Tunisia hadi Italia na malta) imerekodi angalau vifo  3 na kupotea kwa watu 129 mnamo  mwaka 2023,” ameeleza  Chief Charumbira  

Ametaka kukomeswa kwa matumizi ya silaha na badala yake kuimarisha ushirikiano ,umoja na mshikamano wa kidiplomasia baina ya Ulaya na Afrika kwa mstakabali mwema wa Amani na usalama

Ametaka kuwepo ushirikiano  zaidi baina ya bara la Afrika na Ulaya  katika hatua zote za kukabiliana na suala hilo,huku akiutaja umaskini kama chanzo cha uhamiaji haramu ambapo ameomba juhudi zaidi zitakazowezesha kuondoa hali hiyo

Kongamano hilo limeanza  Mei 25,2024 na litahitimishwa Mei 27,2024 kufikiwa kwa maazimio kuhusu uhamiaji

Previous Post Next Post