Ticker

6/recent/ticker-posts

ASKOFU SANGU AWAHIMIZA VIJANA KUSHIRIKI KIKAMILIFU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA IKIWEMO KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI

Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu amewahimiza vijana kushiriki kwa ukamilifu katika zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Ametoa wito huo kwa vijana wakati akizungumza kwenye Misa ya pamoja (Joint Mass) iliyoandaliwa na Umoja wa wanafunzi wa vyuo Tanzania (TMCS) kanda ya Shinyanga ambayo imefanyika katika ukumbi wa chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto.

Askofu Sangu amewasisitiza vijana kutowaaachia wazee pekee yao mchakato wa uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao utafanyika baadaye mwaka huu, na badala yake wanapaswa kutumia haki hiyo kushiriki uchaguzi huo kwa kwenda kupiga kura kuwachagua viongozi wanaowataka na kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo Uenyekiti wa Mtaa,Kitongoji na Kijiji.

Pamoja na wito huo, Askofu Sangu amewataka vijana kujiepusha na vitendo vya rushwa katika kipindi chote cha uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka kesho, kwa kuwa vitendo hivyo ni kinyume cha misingi ya haki na chukizo mbele za Mwenyezi Mungu na vinaikosesha jamii haki ya kupata viongozi bora wanaoweza kutatua changamoto zilizopo ikiwemo kuleta maendeleo.

Askofu sangu amewaonya vijana kamwe kutokubali kutumika vibaya na wanasiasa wenye uchu wa madaraka, wanaowatumia kwa maslahi yao binafsi kuchochea fujo, fitina na mafarakano ndani ya jamii.

“Tunaelekea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka huu ningetamani vijana mjitokeze mchukue fomu kugombea uenyekiti nafasi yoyote ile chukueni fomu, ni wajibu wenu ni haki yenu msiwaachie wazee kwamba ninyi vijana hamuwezi, hapana, kachukueni fomu na wale wenye uwezo wa kupiga kura mkapige kura ni haki yako na niwajibu wako kufanya hivo”.

“Na katika kuelekeza uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwaka kesho sisi kama vijana tusikubali kutumika vibaya hasa kwenye kampeni wanaopandikiza chuki, fitina na mafarakano tuwakemee kabisa hawafai lakini pia wapo baadhi yao wanawaza kutumia rushwa rushwa ni adui wa haki  kwahiyo mtu akikupatia rushwa kwenye sanduku la kura usimpigie kura huyo hafai”amesema Askofu Sangu

Wakati huohuo, Askofu Sangu ameendelea kuwakumbusha Wakristo Wakatoliki kusimama imara katika imani imani yao huhu wakijenga tabia na moyo wa majitoleo katika shughuli mbalimbali za utume wa Kanisa na kijamii.

Mwenyekiti wa Tanzania Movement of Catholic Students (TMCS) kanda ya Shinyanga Musa Jeremiah Mungo, alibainisha mafanikio mbalimbali ya umoja huo ikiwemo changamoto kadhaa, na alimpongeza Askofu Sangu kwa namna anavyojitoa kukutana na kusali na makundi mbalimbali yaliyopo ndani ya Kanisa ikiwemo TMCS.

Tanzania Movement of Catholic Students (TMCS) ni umoja wa wanafunzi wakatoliki wa vyuo na taasisi zote za elimu ya juu nchini Tanzania pia ni chama cha kitume kinachohudumu katika ngazi ya vyuo kadri ya mwongozo wa Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania kikiwa na lengo la kumleta mkristo katika mazingira ya uanafunzi.

Umoja huu umejikita zaidi katika kuwajenga wanafunzi wakatoliki kiroho wakiongozwa na kauli mbiu inayosema “Kipaumbele kwa wahitaji”.

Askofu wa Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akizungumza kwenye sherehe ya Joint Mass ambayo imeandaliwa na Tanzania Movement of Catholic Students (TMCS) kanda ya Shinyanga

Mwenyekiti wa TMCS kanda ya Shinyanga Musa Jeremiah Mungo akisoma  risala ya Tanzania Movement of Catholic Students (TMCS)

Wanaumoja wa TMCS wakiwa ukumbini, Mbele mwenye koti ni Mwenyekiti wa chama cha Vijana Wakatoliti Wafanyakazi (VIWAWA) Jimbo la Shinyanga Mw. Leonard Mapolu ambaye pia ni Mwenyekiti wa VIWAWA taifa

Wanakwaya

Wanavyuo

Viongozi wa TMCS Kanda ya Shinyanga waliochaguliwa hivi karibuni wakiapa mbele ya Askofu Sangu.

Askofu Sangu akipokea zawadi iliyoandaliwa na TMCS kanda ya Shinyanga.

Askofu Sangu akipokea zawadi iliyoandaliwa na TMCS kanda ya Shinyanga.

Askofu Sangu akishukuru kwa zawadi ya TMCS kanda ya Shinyanga

Askofu Sangu akiwa kwenye picha ya pamoja na Makundi mbalimbali

Askofu Sangu akiwa kwenye picha ya pamoja.

Askofu Sangu akisalimiana na watoto wa utoto Mtakatifu Kolandoto

Post a Comment

0 Comments