Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, kesho Jumapili tarehe 02.06.2024, ataongoza Misa takatifu ya Ekaristi takatifu katika Kanisa Kuu la Mama mwenye huruma, Ngokolo mjini Shinyanga.
Kwa mujibu wa Katibu wa Askofu Padre Paul Mahona, Misa hiyo itaanza saa 2:00 asubuhi na itakwenda pamoja na kupokea Komunyo ya kwanza kwa watoto 170.
Domika ya Ekaristi Takatifu huadhimishwa kila mwaka na Kanisa Katoliki kote ulimwenguni, ili kuenzi ukuu wa Sakramenti ya Ekaristi takatifu, yaani Mwili na Damu ya Yesu Kristo.
Post a Comment