ASKOFU WA KANISA KATOLIKI JIMBO LA SHINYANGA MHASHAMU LIBERATUS SANGU AELEZA UKUU WA SAKRAMENTI YA EKARISTI TAKATIFU KWENYE KANISA

 

Askofu wa Kanisa katoliki Jimbo la Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, ameelezea ukuu wa Sakramenti ya Ekaristi takatifu (Mwili na Damu ya Yesu Kristo) kwenye Kanisa na kubainisha kuwa, ndiyo msingi wa Imani Katoliki na madaraja yote yaliyopo ndani ya Kanisa.

Askofu Sangu ametoa mafundisho hayo wakati akiadhimisha Misa ya Dominika ya Ekaristi takatifu katika Kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga, ambayo imekwenda pamoja na kupokea Komnyo ya kwanza kwa watoto 170 wa Parokia hiyo.

Amesema ustawi na uimara wa Kanisa Katoliki unatokana na uwepo wa Sakramenti ya Ekaristi takatifu kwa sababu ndiyo chimbuko la madaraja yote ndani ya Kanisa.

Amesisitiza kuwa, Kanisa  litaendelea kuienzi kwa Imani kubwa Ekaristi takatifu kwa kuwa ndani yake yumo Kristo mwenyewe akiwa mzima.

Askofu Sangu amewasisitiza Wakatoliki kuendelea kuamini nguvu iliyomo ndani ya Sakramenti ya Ekaristi takatifu, na kupitia Sakramenti hiyo wasali kuiombea dunia ili watu wake wawe na upendo, umoja, amani na maelewano na kukoma kwa hali ya magomvi, chuki, vita na mafarakano ili pawe mahali salama pa kuishi.

Amewahimiza kuiishi Sakramenti ya Ekaristi takatifu kwa maneno na matendo yao, wakiiga mfano wa Kristo mwenyewe aliye mpole, mwema na mnyenyekevu.

Leo, Kanisa Katoliki kote duniani linaadhimisha Dominika ya Ekaristi takatifu, ambayo ni siku muhimu ya kutambua na kuenzi ukuu wa Mwili na Damu ya Yesu Kristo kupitia maumbo ya Mkate na Divai.

Askofu Sangu akiwa amebeba Mostrance yenye Sakramenti kuu ya Ekaristi takatifu

Wanakwaya wa Kwaya ya Mtakatifu Cecilia (Kwaya ya Muungano) wakiwa kwenye maandamano kuingia Kanisani

Askofu Sangu na Mapadre wakiwa kwenye Maandamano kuingia Kanisani

Askofu Sangu akiendelea na Adhimisho la Misa

Msomaji wa somo la kwanza akisoma somo

Suzana Masanja akisoma somo la pili

Wanakwaya wakiendelea kuimba Kanisani

Shemasi James Chingila anayefanya utume katika Parokia ya Kanisa kuu Ngokolo akisoma somo la Injili

Askofu Sangu akitoa mahubiri

Waamini wakiendelea na adhimisho la Misa kanisani

Waamini wakiendelea kutoa sadaka

Askofu Sangu akipokea matoleo

Askofu Sangu akiwapatia Komunyo ya kwanza watoto

Askofu Sangu na waamini wakiwa kwenye Maandamano ya Ekaristi


Askofu Sangu akiwa katika kituo cha kwanza cha maandamano ya Ekaristi

Askofu sangu akiwa kwenye kituo cha pili cha maandamano

Previous Post Next Post