Jeshi la
polisi kitengo cha usalama barabarani
Wilaya ya Shinyanga limesema limeendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia sheria, kanuni,na
matumizi sahii ya alama za usalama barabarani ili kuzuia ajali.
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa polisi kitengo cha
usalama Barabarani wilaya ya shinyanaga
ASP Dezidery Kaigwa wakati akizungumza na Misalaba Media ofisini kwake, ilipotaka kujua hatua zinazochukuliwa kwa waendesha baiskeli wanaokiuka sheria za
usalama barabarani ikiwemo vyombo vyao kutokuwa na kengere na taa.
Kaigwa amesema kuwa jeshi hilo limekuwa likitoa
elimu ya usalama barabarani mara kwa
mara kwa watumiaji wa vyombo vya moto,baiskeli pamoja na watembea kwa miguu
na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya
wale wote wanaokiuka sheria ya usalama barabarani.
“Sisi
tumejipanga na tunaendelea kutoa elimu kwa hawa watumiaji wa Baskeli kwahiyi
tunawaelekeza kwamba lazima wazingatie sheria za usalama barabarani pindi
wawapo barabarani hususan wakati wa usiku sambamba na hilo tunawataka
kuhakikisha Baskeli zao zimefungwa taa kwa ajili ya kuonyesha mwanga wanapokuwa
wanaendesha Baskeli zao usiku pamoja na kuwa na kengere na breki za Baskeli ili
wasije wakasababisha ajali wanapokuwa barabarani”.
“Sheria
iko wazi kwa wale ambao wanakiuka sheria basi sheria huchukua mkondo wake kwa
kuwakamata na hili zoezi huwa linaendelea hasa nyakati za usiku kukamata
Baskeli ambazo hazina breki, taa pamoja na refrekta kwahiyo niwatake wale
watumiaji wa Baskeli waendelee kuzingatie sheria za usalama barabarani pia na
watumiaji wengine wa vyombo vya moto na wao wachukulie kwamba hawa watumiaji wa
Baskeli ni sehemu ya barabara kwahiyo wawapo barabarani wasiwe vyanzo vya
kusababisha ajali, ili kuepuka ajali zisizotarajiwa basi watumiaji wote wa barabara
wachukue tahadhari”.
“Nitoa
wito kwa wale wanaotumia aina hii ya usafiri kwa wale ambao ni abiria ukikuta
Baskeli haina refrekta haina breki au haina taa basi uchukue tahadhari ya
kukataa kupanda hiyo Baskeli kwani kupanda Baskeli kunaweza kupelekea kwenda
kupata ajali “.amesema ASP Kaigwa
Kauli ya ASP Kaigwa inafuatia malalamiko ya
baadhi ya wanainchi dhidi ya
waendesha baiskeli zinazosafirisha abiria
maarufu daladala kutokuwa na kengere wala taa hali ambayo waliitaja
inatishia usalama wa abiria wao na watembea kwa miguu.
Kwa upande wake mwenyeketi wa
wilaya wa waendesha baiskeli za kubeba abiria Bwana Mashaka Malugu ameendelea kutumia nafasi yake kuwakumbusha
umuhimu wa kuzingatia sheria za usalama
barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuzuilika .
Uzingatiaji wa sheria za barabarani ni muhimu kwa watumiaji wote wa barabara wakiwemo madereva wa Magari, waendesha Pikipiki, Bajaji , Baiskeli pamoja na watembea kwa miguu ili kuzuia ajali zinazoweza kuzuilika .
Post a Comment