CCM KIBAHA MJINI YATOA TAMKO MAUAJI YA ASIMWE, KATIBU WA CCM TAWI KATA YA MBWAWA



Na Dismas Lyassa, Kibaha Mjini

CHAMA Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha Mjini Mkoani Pwani kimelaani mauaji ya madereva wa bodaboda (almaarufu Maafisa Usafiri)

Kulingana na taarifa iliyolewa leo Jumapili Juni 2024, mojawapo ya mauaji ni yale yaliyotokea kwa Katibu wa CCM Tawi la Miswe Chini, Kata ya Mbwawa, ndugu Sitakiwi Ramadhan Pazi yaliyotokea hivi karibuni.

Tamko hilo lililotolewa na Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kibaha Mjini leo, linasema CCM kinalaani mauaji ya kikatili yaliyofanywa kwa mtoto Asimwe Novat (mlemavu wa ngozi albino) Mkoani Kagera, mwenye umri wa miaka miwili ambaye alitoweka Mei 30 mwaka huu na kupatikana akiwa amefariki huku baadhi ya viungo vya mwili wake vikiwa vimenyofolewa.

“Tunaomba Jeshi la Polisi kuendelea kuchukua hatua stahiki ili sheria ichukue mkondo wake,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kibaha kinatoa pongezi kwa Jeshi la Polisi kwa hatua ambazo limeanza kuzichukua na kuwatia mbaroni baadhi ya watuhumiwa na tunaomba waongeze kasi ili hali hii itoweke kabisa nchini.
Previous Post Next Post