Na Mapuli Kitina Misalaba
Chama
cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Shinyanga kinatarajia kufanya Mkutano
wa hadhara unaolenga kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya Maandalizi ya
Uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika baadaye Mwaka huu Nchini kote
Mkutano
huo unatarajiwa kufanyika leo Ijumaa Juni 14,2024 kuanzia saa tisa Alasili
katika uwanja wa shule ya msingi Town karibu na viwanja vya Zimamoto Kambarage
mjini Shinyanga.
Mwenyekiti
wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emanuel Ntobi ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa
wa Shinyanga na viunga vyake kuhudhuria katika Mkutano huo ambao ameutaja kuwa
ni muhimu kwa kuwa wananchi watapata elimu ya uraia kuelekea mchakato wa
kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na maandalizi ya Uchaguzi
wa serikali za mitaa.
Mkutano huo wa hadhara umeandaliwa na CHADEMA Jimbo la Shinyanga mjini.
MKUTANO WA HADHARA HAUTAFANYIKA TENA KATIKA VIWANYA VYA ZIMAMOTO