Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Town leo Ijumaa Juni 14,2024.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwenyekiti wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi amewahimiza
wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la
kujiandikisha kwenye daftari la makazi pamoja na daftari la kuduma la wapiga
kura ili kushiriki vema katika uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka huu 2024 pamoja
na uchaguzi mkuu Mwaka 2025.
Mhe. Ntobi ametoa wito huo
leo Ijumaa Juni 14,2024 wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ambao
umeratibiwa na CHADEMA jimbo la Shinyanga mjini na kwamba umefanyika katika viwanja
vya shule ya msingi Town.
Amesisitiza wananchi wote
kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi ikiwa ni pamoja na kujiandikisha mapema
katika daftari la makazi na kwamba hatua hiyo itasaidia kuchagua viongozi bora
wanaowataka.
“Wananchi
wa Shinyanga ili mpate viongozi sahihi wenye kupigania maslahi yenu, lazima
mjitokeze kwa wingi kupiga kura siku ya uchaguzi, na mjiandikishe mapema kwenye
daftari la Makazi na daftari la kudumu la mpiga kura, ili mpate fursa ya
kuchagua viongozi mnaowataka na siyo wakuchaguliwa ,”amesema
Ntobi.
“Nampige
kura kwa kuchagua Mtu na siyo Chama na kuna Uongo ambao unazushwa kwamba
mkichagua wapinzani hamuwezi kupata Maendeleo, niwapeni tu mfano mimi
nilipokuwa Diwani wa Ngokolo mbona nilipata Lami na sasa Ngokolo ina Lami, na
zile Kata za CCM hakuna Lami, ikiwamo Kata ya Kambarage,”ameongeza
Ntobi.
Pamoja na mambo mengine Mhe. Ntobi ametumia nafasi hiyo kuitaka
serikali kuongeza ubunifu kwenye vyanzo vya mapato ili kujiepusha na mikopo
ambayo inaweza kurudisha nyuma maendeleo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la
Shinyanga Mjini Bwana Hamisi Ngunila amesema Chama hicho kimejipanga
kuhakikisha kinasimamisha wagombea imara wenye kupigania maslahi ya wananchi katika
kila nafasi ya uongozi.
Naye ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa jimbo la Shinyanga kuendelea kukiunga mkono Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika kupigania haki ya kila mmoja na maendeleo ya taifa.
Misalaba Media imezungumza na baadhi ya wananchi ambao wamehudhuria mkutano huo wameshukuru kwa elimu hiyo huku wakiahidi kuchagua viongozi bora.
Mwenyekiti wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Town leo Ijumaa
Juni 14,2024.
Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Bwana
Hamisi Ngunila akizungumza kwenye
mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Town.
Mwenyekiti wa CHADEMA Jimbo la Shinyanga Mjini Bwana Hamisi Ngunila akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika viwanja vya shule ya msingi Town.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Agatha Mamuya
akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara leo Ijumaa Juni 14,2024.
Katibu wa Chadema Mkoa wa Shinyanga Agatha Mamuya
akizungumza kwenye mkutano huo wa hadhara leo Ijumaa Juni 14,2024.