Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Modest Mkude amewataka
wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la undikishaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga kura pamoja na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Mhe. Mkude ameyasema hayo Tarehe 21 Juni 2024 alipokuwa akifunga
Mashindano ya Mpira ligi ya kata ya Ukenyenge
"Ninashukuru sana
kwa kunialika kuja kufunga Mashindano haya ya ligi ya Kata ya Kunyenge kwa kuwa
mimi ni Mwanamichezo ninayofuraha sana kuzipongeza timu zilizoingia Fainali
timu ya Bulimba na Timu ya Wila ninawatakia Mchezo Mwema wenye ushindani mzuri,
Pia nitumie fursa hii Kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa Wingi pindi
utakapoanza Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura na kushiriki kimalifu
katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 kwani ni haki ya kila mtu kumchagua
kiongozi anayeona anafaa”. Alisema Mkude.
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Ukenyenge Mhe. Underson
Mandia amezipongeza timu zote zilizofika fainaili kwani mashindano hayo
waliyaanzisha kwa lengo la kuhamasisha Wananchi kuutambua Mchakato wa Uchaguzi
ili waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi Uchaguzi 2024.
Naye Katibu Tarafa wa Kata ya Negezi Bw, Omary Mwenda
amesema mashindano hayo yana tija kubwa Sana katika kuhamasisha wanachi
kushiriki kikamilifu katika uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na
kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na kuahidi
kufanya mashindano hayo kila kata ndani ya Tarafa ya Negezi
Aidha katika Mashindano hayo timu ya Wila iliibuka Mshindi
kwa kuiadhibu timu ya Bulimba gori moja ambalo lilifungwa na Mshambuliaji
Anthony Masunga.