Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akijibu kero na mamalamiko mbalimbali ya wakazi wa kata ya Tinde leo kwenye mkutano wake wa hadhara.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro
amewahakikishia wakazi wa kata za Tinde, Iselamagazi na Didia kuwa maombi yao
ya kupunguziwa bei za maji yanashughulikiwa na kwamba siku zijazo wataanza
kulipia bili za maji kama watumiaji wengine wa Manispaa ya Shinyanga.
Ameyasema hayo leo baada ya kupokea kero na
malalamiko mbalimbali kwa wananchi katika mkutano wake wa hadhara ambao
umefanyika katika uwanja wa shule ya msingi Tinde, ambapo wananchi wamesema kuwa
muda mrefu wamekuwa wakilipia Shilingi 2500
unit tofauti na maeneo mengine ya Manispaa ya Shinyanga.
Amesema suala hilo lipo hatua za mwisho ambapo amewatoa
hofu wakazi wa kata za Didia, Iselamagazi pamoja na Didia kuwa siku zijazo
wataanza kulipa bei za maji kama watumiaji wa kata zingine za Manispaa ya
Shinyanga.
“Suala
la maji kwa kifupi limefika hatua za mwisho toka nilipotoa yale maelekezo kwenye
mkutano pale Didia kwamba bei za maji kwenye kata za Iselemagazi, Tinde na
Didia zishushwe kutoka shilingi 2500 kwa Unit mpaka elfu 1400 na kama ambavyo
mjini wanalipa baada ya wananchi kuniambia
zaidi ya Miaka miwili wamekuwa wakilipa elfu 2500 huku mjini wakilipa
elfu 1400 na kwahiyo tulitoa maelekezo lakini
maelekezo yale niliyatoa baada yangu mimi kuwasiliana na Mhe. Mbunge na Mhe.
Waziri Awezo tukakubaliana ndiyo maana kwenye ule mkutano niliwaelekeza EWURA wakamilishe
huo mchakato ambao kwa Miaka miwili umekuwa haukamiliki lakini baada ya agizo
la juzi huo mchakato umeshakamilika”.
“Mara
ya mwisho nilipokuwa Dodoma niliwaziliana tena na Mhe. Awezo nikiwa na Mhe.
Mbunge na tulipofika pale wizarani Mhe, Awezo akatuonyesha amekwisha pokea
barua kutoka EWURA bodi ya EWURA imeidhinisha kushusha bei za maji kwenye kata
za Tinde, Didia na Iselemagazi na baada ya hapo wiki iliyoisha SHUWASA
wamenifuata ofisini wakiwa wamepokea barua kutoka kwa Mhe. Waziri ya agizo la
kushusha hizo bei kwa mujibu wa sheria ile barua inavyotoka kwa waziri
kinachofuatia ni kutangaza kwenye gazeti la serikali”.amesema
DC Mtatiro
Mkuu wa Wilaya huyo akiwa anaendelea na
mkutano wake amempigia simu meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi Mhandisi Walter
Christopher ambaye pia ametoa ufafanuzi kuhusu suala hilo.
“Ombi tayari nimeshapitishwa na bodi ya EWURA la kufanya bei ziwe
sawa katika eneo la Shinyanga sasa hivi
tumeshapeleka kwenye gazeti wakishaturudishia
ndiyo tunatoa kwa ajili ya utekelezaji
kwahiyo tunaimani Mwezi huu wa sita wataanza na hiyo bei ambayo ni sawa na
wengine”amesema Mhandisi Christopher
Pamoja na mambo mengina wakazi wa kata
ya Tinde wametaja changamoto na kero mbalimbali zilizopo ikiwemo changamoto ya
ukosefu wa umeme katika baadhi ya vijiji , stendi pamoja na ukosefu wa maji
katika mnada wa Tinde.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akijibu kero na mamalamiko mbalimbali ya wakazi wa kata ya Tinde leo kwenye mkutano wake wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akijibu kero na mamalamiko mbalimbali ya wakazi wa kata ya Tinde leo kwenye mkutano wake wa hadhara.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Stewart Makali akitolea ufafanuzi kero za wananchi katika mkutano wa hadhara leo.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Stewart Makali akitolea ufafanuzi kero za wananchi katika mkutano wa hadhara leo.Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano huo.