DK. MPANGO AWATAKA WASOMI KUWA NA CHACHU UPATIKANAJI DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO

 

Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango wakati akifungua kongamano la kwanza la kitaifa kuhusu maandalizi ya dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050, lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo, Jumamosi Juni 8, 2024.

Dar es Salaam.
Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ametaja mambo makuu matano, ikiwemo tatizo la ajira kwa vijana akisema ni muhimu yakafanyiwa tafakuri na wanazuoni pamoja na wananchi ili kuingizwa katika maandalizi ya dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050.

Akizungumza mapema leo, Jumamosi Juni 8, 2024 wakati akifungua kongamano la kwanza la kitaifa kuhusu maandalizi ya dira ya Taifa ya maendeleo ya mwaka 2050, lililofanyika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Amesema dira ya mwaka 2050 inapaswa zaidi kuwa ya vijana kwa ajili ya vijana, kwa sababu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 imebainisha wazi kuwa asilimia 77.5 ya Watanzania ni vijana na watoto kati ya miaka 0-35. Huku kundi la vijana kuanzia miaka 15-35 wakiwa asilimia 34.5.
Previous Post Next Post