Manispaa ya Shinyanga imeshika nafasi ya 18 katika utoaji wa taarifa kwa Umma kupitia tathimini iliyofanywa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuangalia namna wizara, Taasisi sekretarieti za Mikao na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kutoa taarifa kwa Umma kwa kipindi cha mwaka 2023/2024.
Ambapo Halmashauri 20 zimefanya vizuri Kati ya 184 katika utoaji wa taarifa kwa umma ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya awamu ya sita.
Utoaji wa Tuzo pamoja na cheti cha pongezi zimetolewa leo tarehe 21 Juni, 2024 na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye katika kikao kazi cha 19 cha Maafisa Habari wa Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jiji Dar-es-salaam .