HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA NAYO YAPATA HATI SAFI, MKUU WA MKOA MHE. MACHA APONGEZA KWA MAMBO MATATU

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kupata hati safi kutokana na kujibu hoja za mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) kwa Mwaka wa fedha 2022\2023.

Ameyasema hayo leo Jumanne Juni 25,2024 wakati akifunga kikao cha baraza maalum la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga lililojadili taarifa za utekelezaji wa majibu ya hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG.

RC Macha pamoja na mambo mengine ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kupata hati safi kuhu akihimiza kuendeleza ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

“Kwanza niwapongeza mstahiki meya pamoja na mkurugenzi kwa sababu mna tuzo tatu za siku za hivi karibuni, kwanza kwa kupata tuzo ya kuwa Manispaa safi kwa Mwaka 2023 kuliko Manispaa zote 19 za hapa nchini, lakini pia Manispaa hii ni kati ya Manispaa zinazojitahidi kutoa taarifa kwa waandishi wa habari katika Halmashauri 184 hii niya 18 Manispaa hii ni kati Manispaa bora kutoa taarifa kwa waandishi wa habari katika shughuli zinazofanywa kwenye Manispaa hii lakini jambo la tatu ni hili la kuwa miongoni mwa Halmashauri zilizopata hati safi kwahiyo haya mambo matatu hahaji tu hivi hivi kuna watu wanashughulika kwahiyo mstahiki meya na madiwani wake pamoja na mkurugenzi na watendaji wake wote niwapongezeni sana”.amesema RC Macha

Pia Mhe. Macha ametumia nafasi hiyo kuwataka watendaji wote wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kuendelea kufanya kazi kwa bidii, juhudi na maarifa ili kuongeza  tija na ufanisi.

Akiwasilisha taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa hesabu zilizokaguliwa katika Mwaka unaoishia terehe 30 Juni, 2023 mkuu wa kitengo cha fedha na uhasibu Manispaa ya Shinyanga Bwana Mulokozi Kishenyi ameitaja  Halmashauri hiyo kupata hati safi 2023.

“Katika hesabu zilizofungwa kwa kipindi cha kuishia tarehe 30, Juni 2023 Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilipata hati safi ya ukaguzi aidha kutokana na ukaguzi huo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilikuwa na jumla ya hoja 43 ambazo kati ya hoja hizo, hoja 13 zilikuwa za Miaka ya nyuma na hoja 30 zilikuwa za Mwaka 2022\2023 Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga imeendelea kutekeleza hoja zilizoibuliwa na hati safi ambapo hadi sasa jumla ya hoja 7 zimetekelezwa kikamilifu na kufungwa na hoja 36 utekelezaji wake unaendelea”.amesema Kishenyi

Kwa upande wake mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amesisitiza kuongeza umakini na ushirikiano katika utatuzi wa hoja zinazoibuliwa mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG ili kuepusha mkanganyiko.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Anord Makombe pamoja na mambo mengine ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha madiwani kwenda kuhamasisha wananchi kufanya maandalizi sahihi ya kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka huu 2024 pamoja na uchaguzi mkuu 2025.

Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Juni 25,2024  limefanya kikao maalum kujadili taarifa za utekelezaji wa majibu ya hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG.

Mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akishiriki kwenye kikao cha baraza maalum la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga lililojadili taarifa za utekelezaji wa majibu ya hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG leo Juni 25,2024.


 

Previous Post Next Post