HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA KWA KUSHIRIKIANA NA BARAZA LA WATOTO YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO WA AFRIKA DUNIANI

Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Rehema Edson akizungumza kwenye maadhimishio ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani, katika kongamano la watoto Halmashauri ya Manispaa ya  Shinyanga. 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na baraza la watoto imeadhimisha siku ya mototo wa Afrika Duniani ambayo huadhimishwa  kila Mwaka, na kwamba kilele chake ni Juni 16.

Katika maadhimisho hayo limefanyika kongamano la watoto pamoja na shughuli mbalimbali ikiwemo maonesho ya kazi za watoto ikiwa ni sehemu ya kutambua umuhimu wa siku hiyo na kutoa fursa kwa watoto wote wa Halmashauri hiyo.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi wa serikali na taasisi binafsi wakiwemo wadau wa kutetea haki za watoto ambapo kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mototo wa Afrika Duniani kwa Mwaka huu 2024 inasema “ELIMU JUMUISHI KWA WATOTO: IZINGATIE MAARIFA, MAADILI NA STADI ZA KAZI”.

Akizungumza mgeni rasmi katika kongamano la watoto, afisa maendeleo wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Rehema Edson amewapongeza watoto kwa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya mototo wa Afrika huku akiwataka kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia maadili mema.

“Kwanza niwapongeze watoto kwa ushiriki wenu na kwa namna ambavyo unatambua haki zenu lakini niwataka kutimiza wajibu wenu, mkumbuke sana mnaowajibu kwa wazazi kwa watu wazima mnawajibu kwa walimu mnawajibu kwa viongozi kwahiyo wakati mnasema haki kumbuka kabisa haki yako inaweza isiwe haki kama wewe haujatimiza wajibu”.

“Kauli mbiu ya Mwaka huu inasisitiza kuzingatia maarifa, maadili na stadi za kazi kwahiyo zingatieni stadi za kazi zingatieni maadili mema kuweni raia wema kuweni watoto wema kuweni waumini wema nyumbani mkipewa kazi na wazazi sasa hivi mpo likizo fanyeni achene kuzurula na Mungu atawasaidia sana kutimiza ndoto zenu”.amesema Rehema

Akizungumza Polisi jamii kutoka dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Shinyanga Jane Mwazembe ametoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia na njia za kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili.

Amewasisitiza watoto  kutoa taarifa  wanapoona dalili za ukatili ambapo amewataka kutoa taarifa  kwa mtu yoyote ambaye wanamwamini wakiwemo wazazi, walimu, maafisa ustawi wa jamii, pamoja na kutoa taarifa kwenye serikali za mitaa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la watoto Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza hilo Taifa Raphael Charles amewahimiza wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto huku akisisitiza  kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya elimu ambayo ni muhimu katika maisha yao ya kila siku.

Mwenyekiti huyo ametumia nafasi hiyo pia kuipongeza serikali kwa kuendelea kuthamini haki za watoto hali ambayo imesababisha kuimarishwa kwa huduma za kiafya kwa watoto, wakati huo huo ameiomba serikali kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili watoto.

Leo ni kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani ambapo kilele cha maadhimisho hayo  kimkoa   yanatarajiwa kufanyika Juni 19 wiki ijayo siku ya Jumatano katika kata ya Didia Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Rehema Edson akizungumza kwenye maadhimishio ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani, katika kongamano la watoto Halmashauri ya Manispaa ya  Shinyanga. 

Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Rehema Edson akizungumza kwenye maadhimishio ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani, katika kongamano la watoto Halmashauri ya Manispaa ya  Shinyanga. 

Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Rehema Edson akizungumza kwenye maadhimishio ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani, katika kongamano la watoto Halmashauri ya Manispaa ya  Shinyanga. 

Mwenyekiti wa baraza la watoto Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza hilo Taifa Raphael Charles akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Mwenyekiti wa baraza la watoto Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza hilo Taifa Raphael Charles akizungumza kwenye maadhimisho hayo.

Afisa ustawi wa jamii wa Manispaa ya Shinyanga Elizabeth Mweyo akitoa mada yake inayosema wajibu na majukumu ya mtoto akiwa ndani na nje ya shule.

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani yakiendelea mjini Shinyanga.

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani yakiendelea mjini Shinyanga.

Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Duniani yakiendelea mjini Shinyanga.

Mwenyekiti wa Asasi ya Wanawake laki moja Mkoa wa Shinyanga Annaskolastika Ndagiwe ( MC Mama Sabuni) akitoa mada inayohusu ulinzi na usalama wa mtoto akiwa ndani na nje ya shule.  

Mwenyekiti wa Asasi ya Wanawake laki moja Mkoa wa Shinyanga Annaskolastika Ndagiwe ( MC Mama Sabuni) akitoa mada inayohusu ulinzi na usalama wa mtoto akiwa ndani na nje ya shule.  

Previous Post Next Post