Na Mapuli Kitina Misalaba
Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta ghafi Tanzania
(EACOP) leo wametoa semina ya siku moja kwa waandishi wa habari Mkoa wa
Shinyanga kuhusu hatua mbalimbali za maendeleo ya mradi huo.
Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa Empire mjini
Shinyanga ambapo mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwenye mradi huo Bi. Catherine
Mbatia amesema mpaka sasa mradi huo umefikia takribani asilimia 29 na kwamba
shughuli zinaendelea katika maeneo
mbalimbali Nchini.
Amesema mradi huo umefikia takribani asilimia 99 katika hatua za ulipaji fidia kwa wananchi huku akieleza kuwa suala la ajira linazingatiwa zaidi akwa kupewa kipaumbela wazawa wa eneo husika kama sehemu
ya kuwainua kiuchumi.
“Mpaka
sasa hivi mradi umeshafikia takribani asilimia 29 na shughuli zinaendelea
katika maeneo mbalimbali lakini katika ulipaji wa fidia tumeshafikia zaidi ya
asilimia 99 hamna mtu ambaye mradi wake utapotea katika mradi mafanikio ya wazi
ambayo kila mtanzania ni rahisi kuyaona ni ajira kuna kitu tunaita local
content ambacho kinawashirikisha wazawa kwahiyo kama kuna kazi hapa Shinyanga
inayohusiana na mradi mtu wa kwanza atakayefikiriwa kupata kazi hiyo ni mzawa
wa hapa Shinyanga hiyo ni faida moja wapo kubwa sana lakini pia patachamgamsha
maendeleo ya hapa Shinyanga kwa sababu kutakuwa na mzunguka wa fedha”.
“Mradi huu unatoa fursa mbalimbali za kiuchumi na kibiashara
katika hatua za awali za mradi (early works), wakati wa ujenzi (Construction)
na wakati wa uendeshaji wa mradi (operations), Mradi pia unatoa fursa kwa
watanzania kupitia makampuni ya watoa huduma kujiandikisha katika kanzi data ya
EWURA ambaye ni mdhibiti wa mkondo wa chini na kati katika sekta ya uziduaji na
vilevile kwa watanzania kujiandikisha kupitia kanzidata ya nguvukazi iliyopo Ofisi
ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu kupitia kitengo cha
TaESA”. amesema Bi. Catherine
Afisa mawasiliano wa nje EACOP nchini Tanzania Bwana
Abbas Nassoro Abraham amesema mradi wa bomba la mafuta nchini Tanzania utapita
katika Mikoa nane ambayo ni Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida,
Dodoma, Manyara pamoja na Tanga.
Bwana Abraham ametumia naafsi hiyo kuwakumbusha wananchi
kuendelea kuunga mkono jitihada zinazofanyika katika utekelezaji wa mradi wa
bomba la mafuta ghafi ikiwa ni pamoja na kulinda miundombinu katika maeneo
ambayo bomba hilo linapita.
Kwa upande wake mratibu wa mahusiano ya jamii EACOP
Mkoa wa Shinyanga Bi. Cecilia Nzeganije amesema mradi wa bomba la mafuta kwa Mkoa
wa Shinyanga umepita katika Wilaya ya Kahama na kwamba zaidi ya watu mia sita
wamenufaika na mradi huo.
“Urefu
wa bomba ni kilomita 54.72 kilomita hizo zinapita kwenye kata nane (8) pamoja
na vijiji na mitaa 16 ambapo kwa eneo hili la kilomita 54. 72 tunaidadi ya waguswa 619 katika hawa wote
waguswa 619 utwaaji wa ardhi umekamilika kwa silimia 99 kwa sababu waguswa 609
tayari wamekwisha pokea malipo yao ya fidia kwa mujibu wa sheria na wengine kumi ni wale wenyechangamoto na
wengina wamesafiri ama kuna kesi kwenye mabaraza la ardhi ambapo hawa mchakato
wao utakamilika mara tu baada ya kukamilisha au kutatua changamoto zilizopo”.
“Lakini
pia kwenye Wilaya ya Kahama tunawaguswa 12 ambao walipoteza makazi yao lakini
katika hao 12, kumi walichagua kujengewa nyumba wakati wawili walichagua
kulipwa fedha ili waende wakajenge wenyewe, wale ambao walichagua kujengewa
nyumba ambao ni 10 tayari wamejengewa
nyumba lakini zimejengwa nyumba 12 kwa Wilaya ya Kahama ambapo yatari waguswa hawa walikabidhiwa
nyumba zao mwaka jana Mwezi wa nane walikabidhiwa nyumba zao na mkuu wa Wilaya
ya Kahama na kupewa muda wa matazamia ya Mwaka mmoja kwamba wakipata changamoto
yoyote basi mradi unawatumia wakandarasi wake kurekebisha changamoto bure”.
“Pia
Wilaya ya Kahama tulikuwa na makaburi 25 na yote yamehamishwa na uhamishwaji
huo wa makaburi ulihusisha mila na desturi za familia zinazomiliki makaburi
hayo hakukuwa na changamoto yoyote maana yote yaliweza kuhamishwa salama,
sambaba na hayo pia tunazoezi la kuendelea kuwapatia chakula wakuswa zoezi hilo
lilianza Mwaka jana Mwezi wa kumi lakini tunawataalam mbalimbali kutoka
Manispaa ya Kahama ambao ni watumishi wa serikali ambao tunafanya nao kikao
kila robo ya Mwaka tunajadili kwa pamoja
kwamba tufanye nini lakini pia tunamfumo wa kupokea, kusikiliza na kutatua
malalamiko ya watu”.amesema Bi. Cecilia
Nao baadhi ya waandishi wa habari kutoka Klabu ya
waandishi wa habari ( SPC) Mkoa wa Shinyanga wamepongeza na kushukuru kwa
semina hiyo ambapo wameahidi kutumia kalamu zao kuelimisha jamii juu ya hatua mbalimbali zitakazokuwa zinafikiwa
katika mradi huo.
Bomba la Mafuta la Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), Huu ni mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki
(EACOP) kutoka Kabaale – Hoima nchini Uganda kwenda kwenye peninsula ya Chongoleani
mkoani Tanga nchini Tanzania.
Mradi
huu una urefu wa jumla ya kilomita 1443 kati ya hizo kilomita 296 zipo nchini
Uganda na kilomita 1147 zipo Tanzania na kwamba Bomba hilo vilevele linapita
katika Mikoa 8 lakini pia wilaya 24, kata 134 na vijiji zaidi ya 180.
Lengo la mradi huu ni kuwezesha mafuta yatakayozalishwa nchini Uganda kusambazwa katika soko la ndani na sehemu inayobaki kuuzwa nje kwenye soko la kimataifa kupitia bomba la mafuta.
Mkuu wa
kitengo cha mawasiliano kwenye mradi wa EACOP, Bi. Catherine Mbatia akizungumza
kwenye semina na waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga leo Juni 7, 2024.
Afisa mawasiliano wa nje EACOP nchini Tanzania Bwana
Abbas Nassoro Abraham akiwasilisha mada yake kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa
Shinyanga katika ya semina ya leo Juni 7,2024.
Mratibu wa mahusiano ya jamii EACOP Mkoa wa
Shinyanga Bi. Cecilia Nzeganije akieleza hatua mbalimbali za maendeleo katika mradi
wa bomba la mafuta ghafi katika Wilaya ya Kahama.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa
katika semina iliyoandaliwa na Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta ghafi
Tanzania (EACOP) leo mjini Shinyanga.
Afisa mawasiliano wa nje EACOP nchini Tanzania Bwana
Abbas Nassoro Abraham akiendelea kuwasilisha mada yake kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa
Shinyanga katika ya semina ya leo Juni 7,2024.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa
katika semina iliyoandaliwa na Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta ghafi
Tanzania (EACOP) leo mjini Shinyanga.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa
katika semina iliyoandaliwa na Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta ghafi
Tanzania (EACOP) leo mjini Shinyanga.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa
katika semina iliyoandaliwa na Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta ghafi
Tanzania (EACOP) leo mjini Shinyanga.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa
katika semina iliyoandaliwa na Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta ghafi
Tanzania (EACOP) leo mjini Shinyanga.
Afisa mawasiliano wa nje EACOP nchini Tanzania Bwana
Abbas Nassoro Abraham akiwasilisha mada yake kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa
Shinyanga katika ya semina ya leo Juni 7,2024.
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa
katika semina iliyoandaliwa na Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta ghafi
Tanzania (EACOP) leo mjini Shinyanga.
Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta ghafi Tanzania
(EACOP) wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
leo Ijumaa Juni 7, 2024.
Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta ghafi Tanzania
(EACOP) wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga
leo Ijumaa Juni 7, 2024.