IGP WAMBURA - JESHI LA POLISI LIMEWEKEZA KWENYE JAMII ILI KUBAINI, KUTANZUA NA KUZUIA UHALIFU

 Jeshi la Polisi limeendelea kuwekeza kwenye jamii ili kuweza kubaini, kutanzua na kuzuia uhalifu kwenye maeneo mbalimbali ambapo wananchi Pamoja na viongozi wa mtaa wametakiwa kuendelee kushirikiana na Wakaguzi wa kata katika kudhibiti uhalifu.

Kauli hiyo imetolewa na MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura wakati akiwavalisha nishani maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 246 kutoka kanda ya Kusini yenye mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kwa niaba ya Mheshimiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amelimwagia sifa na Pongezi Jeshi la Polisi nchini kwa kuendelea kuimarisha hali ya usalama ya Mkoa huo na wananchi kuendelea kufanya shughuli zao katika hali ya usalama na amani.

Amesema vyombo vya ulinzi vimeendelea kuhakikisha Mtwara inakuwa salama na hata wananchi na makundi mengine mbalimbali wanakaribishwa kuja kuwekeza katika mkoa huo ambao ni rafiki kwa uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Huku akitoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi pamoja na vyombo vingine vya ulinzi na usalana ili kudumisha amani iliyopo umoja na mashirikiano ambayo ni nyenzo thabiti ya maendeleo.


Previous Post Next Post