JKT YATOA WITO VIJANA AMBAO HAWAKURIPOTI MAFUNZO YA LAZIMA KURIPOTI HARAKA MAKAMBINI

 


MKUU wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akizungumza na Waandishi wa habari  Juni 22,2024 katika Ukumbi wa Mabeyo Complex jijini Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele,kuhusu nyongeza ya awamu ya pili ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya Kidato cha Sita mwaka 2024 kujiunga na Jeshi hilo ili kufanya mafunzo hayo ya lazima.

Na Gideon Gregory, Dodoma.

JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limewakata vijana wote waliohitwa awamu ya kwanza kujiunga na Jeshi hilo ambao hawajaripoti makambini mpaka sasa waripoti mara moja katika makambi yaliyo karibu na makazi yao.

Hayo yameelezwa leo Juni 22,2024 Jijini Dodoma na Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena wakati akizungumza na Waandishi wa habari huku akiongeza kuwa wametoa nyongeza ya awamu ya pili ya majina ya vijana waliohitimu elimu ya Kidato cha Sita mwaka 2024 kujiunga na Jeshi hilo ili kufanya mafunzo hayo ya lazima.

"Orodha kamili ya majina ya vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo hayo awamu ya pili na vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo inapatikana katika tovuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz",amesema.

Ameongeza, "Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa hivi karibuni alitoa wito kwa vijana wahitimu wa elimu ya kidato cha Sita mwaka 2024 kujiunga na mafunzo ya JKT kwa lazima (mujibu wa sheria) kwa mwaka 2024, vijana hao walitakiwa kuripoti makambi ya JKT walipopangiwa kuanzia Juni 1,2024 hadi Juni 7,2024 wakiwa na vifaa vilivyoainishwa na JKT kuripoti navyo makambini.

Aidha ameongeza kuwa vijana wote ambao hawajaripoti wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia Juni 22,2024 hadi Juni 26,2024.

Amesema Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana waliohitimu kidato cha Sita mwaka huu kuungana na vijana wenzao ili kujengewa uzaIendo, umoja na utayari wa kulijenga na kulitumikia taifa lao.
Previous Post Next Post