Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA SIASA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI MITANO YA MAENDELEO


Na Mapuli Kitina Misalaba

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga vijijini ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini, Mhe. Edward Ngelela imetembelea na kukagua miradi mitano (5) ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Ziara hiyo imefanyika leo Juni 4, 2024 ambapo miradi iliyotembelewa ni mradi wa matengenezo ya barabara ya Mwawaza – Iselamagazi, mradi wa maji Ng’wampangabule – Sumbigu na Zumve, mradi wa ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Pandagichiza, mradi wa jingo la utawala pamoja na mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Iselamagazi Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga vijijini pamoja na mambo mengine haijaridhishwa na utekelezaji katika mradi wa ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum  shule ya msingi Iselamagazi ambapo kamati hiyo imemuelekeza mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kuchukua hatua za haraka kwa mafundi pamoja na kamati ya ujenzi wa bweni hilo ili liweze kukamilika kwa wakati.

Ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Iselamagazi  unatarajiwa kukamilika Juni 24 Mwaka huu ambapo mpaka sasa ujenzi wa mradi huo upo kwenye hatua za  boma na kwamba umesimama kwa kile kinachoelezwa kuwa fundi yupo Mwanza kwenye halusi kwa muda mrefu sasa.

Kamati hiyo wakati ikitembelea na kukagua hatua za mradi wa matengenezo ya barabara ya Mwawaza – Iselamagazi meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Samson Gechamet wakati akisoma taarifa yake amesema gharama za mradi huo ni zaidi ya Milioni 75 ambapo amesema mpaka sasa mradi upo katika hatua za umwagaji wa vifusi na ushindiliaji.

“Barabara ya Mwawaza – Iselamagazi ni barabara inayoziunganisha kata za Mwantini na Iselamagazi barabara hii inajumla ya urefu wa km 30. 26 utekelezaji wa matengenezo ya barabara hii kwa Mwaka 2023 – 2024 ni uchongaji wa barabara kim 9, kuweka changarawe km 4 na ujenzi wa makalvati 2”.

“Lengo la mradi huu ni kuboresha miundombinu ya barabara ili iweze kupitika na kurahisisha huduma za usafirishaji mpaka sasa utekelezaji wa matengenezo ya barabara hii upo katika hatua za umwagaji wa vifusi na ushindiliaji ambapo matengenezo ya barabara hii yana gharama ya Milioni 75, 230, 400.00 mradi huu unatarajiwa kuleta urahisi wa upitikaji wa barabara kwa wananchi wanaotumia hasa kuelekea makao makuu ya Halmashauri Iselamagazi’.amesema Mhandisi Samson Gechamet

Pia kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Shinyanga vijijini imewataka wasimamizi wa miradi hiyo kusimamia vizuri huku ikiwasisitiza watekelezaji wa miradi kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na kwa kiwango kinachostahili ili wananchi waweze kunufaiska

Meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Samson Gechamet  akikabidhi taarifa yake kwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini, Mhe. Edward Ngelela

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini, Mhe. Edward Ngelela akitoa maelekezo kwa  Meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Samson Gechamet  

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga vijijini, Mhe. Edward Ngelela akitoa maelekezo kwa  Meneja wa wakala wa barabara za mijini na vijijini (TARURA) Wilaya ya Shinyanga Mhandisi Samson Gechamet  

 

Post a Comment

0 Comments