KAMATI YA UTEKELEZAJI UWT WILAYA YA SHINYANGA VIJIJINI YAHAMASISHA WANAWAKE KUGOMBEA NAFASI MBALIMBALI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

Mwenyekiti wa  UWT Wilaya ya Shinyanga vijijiji Bi. Mektrida Kenuka akizungumza.

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mwenyekiti wa umoja wa wanawake wa Chama Cha Mapinduzi UWT Wilaya ya Shinyanga vijijiji Bi. Mektrida Kenuka amewahimiza wanawake katika Wilaya hiyo kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika badae Mwaka huu huku akisisitiza wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Ameyasema hayo kwenye ziara ya kamati ya utekelezaji ya UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini ikiongozwa na Mwenyekiti huyo na kwamba imetembelea kata ya Lyabukande, Lyamidati pamoja na kata ya Ilola kwa lengo la kuhamasisha uhai wa chama na jumuiya.

Bi. Kenuka amewahimiza wanawake hao kujitokeza kwa wingi wakati wa zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la makazi pamoja na daftari la kuduma la wapiga kura ili kushiriki vema katika uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka huu 2024 pamoja na uchaguzi mkuu Mwaka 2025.

“Sasa hivi siyo wakati wa kukaa umeisha nawaomba sana tutoke kwenye kata zetu totoke kwenye matawi yetu tukasemee mazuri yote yaliyofanywa na Rais wetu yapo mambo mengi ameyafanya Rais wetu ametujengea madarasa kwenye shule, ametujengea Hospitali, ametujengea mabarabara kwa kweli Rais ametufanyia mambo mazuri sana tunatakiwa tumuunge mkono kwa asilimia mia moja”.

“Pia mwenyekiti wetu wa UWT Taifa Marry Chatanda alitembea mikoa yote akitusemea sisi akina mama tusiame kwahiyo wakati utakapofika wa kuchukua fomu tuchukue tuache kuogopa kwamba mimi siwezi kuwa kiongozi, mwanamke akiwa kiongozi wanawake wengine hawezi kuwa na shida kwa kuwa kero na changamoto zitakuwa zinatatuliwa haraka kwahiyo akina mama tusilale sana wakati huu ni wakati wetu tumuungeni mkono Rais wetu lakini pia wagumbe wetu wa viti maalum pamoja na madiwani wetu nawaomba sana akina mama tusirudi nyuma wakati huu ni wakati wa kusonga mbele

Kwa upande wake katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini Bi. Magreth Dodoma pamoja na mambo mengine amewasisitiza wanawake kuendelea kukemea ukatili wa kijinsia ikiwemo kutoa taarifa za ukatili unaoendelea kufanyika hasa kwa wanawake na watoto kwa lengo la kuimarisha usalama wa maisha yao.

“Wanawake tunatakiwa tujiamini kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa tuchukue fomu za kuomba naafsi mbalimbali tusiogope lakini pia tuwatembelee wanawake wengine ambao wanasifa za kuwa viongozi lakini wao hawajui kwahiyo tuwatembeleea ili kuwahamasisha kugombea na tuhakikishe tunawaunga mkono ili tuendelee kuchukua dola kila kila vitongoji, vijiji na mitaa”.

“Kingine ni kuhusiana na ukatili wa kijinsia nawaomba wanawake wenzangu tusiwafumbie macho watu wanaofanya ukatili wa kijinsia tuwaseme hadharani lakini pia tukae na watoto wetu na tuwaeleza kwamba haya mambo hapo na tunayasikia kwenye vyombo vya habari watoto wanaingiliwa kinyume na maumbile wewe ni mzazi usifiche maana kuna wengine wanaona aibu wanamaliza kesi za ukatili chini chini wao wenyewe tu kumbe motto ameathirika kisaikolojia mwisho wa siku kijana wako wa kiume anageuka anakuwa mwanamke na sauti anabadilisha kumbe wewe haukumjenga tangu mdogo kwahiyo nawaomba sana mama zangu tukemee vitendo hivyo”.

Wakizungumza na Misalaba Media baadhi ya wanawake wa UWT kutoka kata mbalimbali wameahidi kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo ikiwemo kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Kamati ya utekelezaji ya UWT Wilaya ya Shinyanga vijijini ikiongozwa na Mwenyekiti wake imetembelea kata ya Lyabukande, Lyamidati pamoja na kata ya Ilola kwa lengo la kuhamasisha wanawake kushiriki vema kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa Mwaka huu 2024  pamoja na uchaguzi mkuu Mwaka kesho 2025.

Mwenyekiti wa  UWT Wilaya ya Shinyanga vijijiji Bi. Mektrida Kenuka akizungumza na baadhi ya wanawake wa UWT kutoka kwenye matawi mbalimbali Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.






Previous Post Next Post