Na Mapuli Kitina Misalaba
Kuelekea tamasha la utamaduni wa Msukuma Shinyanga, taasisi
ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION imefanikisha
marekebisho ya kupaka rangi katika jengo la ofisi ya Mahakama ya mwanzo mjini
Shinyanga.
Akizungumza Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY
LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) amesema
tamasha la utamadun wa Msukuma hufanyika kila Mwaka na kwamba kabla ya tamasha
hilo hufanyika shughuli mbalimbali zikiwemo za kijamii.
Mr. Black ameelezea zaidi kuwa Mwaka huu 2024 pamoja
na mambo mengine imefanyika shughuli ya kuboresha jengo la Mahakama ya mwanzo
mjini Shinyanga kwa kupaka rangi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho kuelekea kilele
cha SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL SEASON 3.
Mkurugenzi huyo Mr. Black amesema pamoja na
maboresho katika jengo la Mahakama ya Mwanzo mjini, taasisi THE BSL INVESTMENT COMPANY
LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION kwa kushirikiana na serikali imepanda miti
zaidi ya 30 katika eneo la Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu
ya utunzaji wa mazingira.
“Kupitia
tamasha hili kila Mwaka tumekuwa tukiandaa shughuli mbalimbali kabla ta tukio
husika ukijaribu kuangalia Miaka ya nyuma kuna mambo mbalimbali ya kijamii
ambayo tumeyafanya ikiwemo marekebisho ya miundombinu mbalimbali lakini pia
uwezeshaji katika sehemu mbalimbali na Mwaka huu tumejikita kurekebisha jengo
la Mahakama ya mwanzo ya mjini kulikuwa na uchakavu kidogo wa kuta za nje upande
wa rangi tukaona ni vyema sisi wadau wa maendeleo Mkoa wa Shinyanga tuweze kuweka
mkono wetu kufanikisha jambo hili ikiwa ni shukurani yetu na sadaka yetu kuelekea
tamasha la utamaduni wa Msukuma”.
“Asili
yetu ni uwoto wa asili tumeshiriki pia katika kupanda miti ambapo tumepanda
miti zaidi ya 30 katika eneo linalozunguka Mahakama hii kwa lengo la
kutengeneza kivuli na miti ya matunda lakini pia kuuendeleza uwoto wa asili wa
Mkoa wa Shinyanga”.amesema Mr. Black
Hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Shinyanga Yusuph
Zahoro ameishukuru taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE
LIVE FOUNDATION huku akimpongeza Bwana Peter Frank (MR. BLACK) kwa kufanikisha
ukarabati wa jengo la Mahakama ya mwanzo mjini kwa kupaka rangi.
“Sisi
tunashukuru sana kuwa sehemu ya wanufaika wa tamasha la utamaduni wa Msukuma lakini
kwa dhati kabisa niishukuru kampuni hii ya BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE
LIVE FOUNDATION kupitia mkurugenzi wake Bwana Peter Frank alimaarufu MR. BLACK
kwa safari hii kutuona na sisi Mahaka ya Wilaya ya Shinyanga kuwa wanufaika wa
tamasha hili kwa kupaka rangi jengo hili limependeza kwahiyo tunashukuru sana,
kwa niaba ya uongozi wa Mahakama ndani ya Wilaya ya Shinyanga tunaahidi kabisa
ushiriki wetu usiokuwa wa mashaka tutakuwa wote katika tamasha mwanzo mpaka
siku ya mwisho”.amesema Zahora
Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha maliasili na
hifadhi ya mazingira Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga naye
ameipongeza taasisi ya BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE
FOUNDATION kwa ubunifu wao katika shughuli za kijamii ambapo amesema kuwa
serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika shughuli hasa za
kijamii zinazogusa sekta mbalimbali hasa katika kulina na kuendeleza utamaduni
wa Mkoa wa Shinyanga.
Naye mhifadhi misitu wa Wilaya ya Shinyanga kutoka
taasisi ya Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Bwana Fabian Balele ameipongeza
taasisi ya BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION kwa
kupanda miti ikiwa ni sehemu ya uhifadhi wa misitu ambapo amesema TFS
itaendelea kushiriki kikamilifu katika tamasha la utamaduni wa Msukuma.
Tamasha la utamaduni wa Msukuma (SHINYANGA SUKUMA
FESTIVAL SEASON 3, ambalo limeandaliwa na THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED
AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Mwaka huu 2024 litafanyika kwa siku mbili kuanzia
Jumamosi Juni 29 hadi Jumapili Juni 30.
Mr. Black ametumia nafasi hiyo kuwakaribisha wadau
na wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi ambapo amesema
yatafanyika maonyesho ya Biashara, sanaa, ngoma za asili, burudani pamoja na
Nyama choma”.
Tamasha hilo la utamaduni wa Msukuma litafanyika
katika viwanja vya Nhelegani kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga na kwamba
hakuna kingilio “SHINYANGA SUKUMA
FESTIVAL SEASON 3, LEJIGUKULU LYA NZENGO”.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika siku ya kufungua tamasha la utamaduni wa Msukuma
Jumamosi Juni 29,2024.
Naibu katibu mkuu wizara ya utamaduni, sanaa na
michezo Dkt. Suleiman Serera anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya kufunga
tamasha la utamaduni wa Msukuma Jumapili Juni 30,2024.
Kauli mbiu ya tamasha la utamaduni wa Msukuma kwa Mwaka huu inasema “UTAMADUNI WETU URITHI WETU, SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA MAENDELEO YA TAIFA”
Zoezi la kupanda miti katika eneo la Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga likiendelea na kwamba imeandaliwa na taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la utamaduni wa Msukuma.
Zoezi la kupanda miti katika eneo la Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga likiendelea na kwamba imeandaliwa na taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la utamaduni wa Msukuma.
Hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Shinyanga Yusuph Zahoro akipanda mti katika eneo la Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga na kwamba miti hiyo imeandaliwa na taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la utamaduni wa Msukuma.
Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) .
Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) akipanda mti katika eneo la Mahakama ya mwanzo iliyopo Nguzonane mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la utamaduni wa Msukuma.
Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) akipanda mti katika eneo la Mahakama ya mwanzo iliyopo Nguzonane mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la utamaduni wa Msukuma.
Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) akimwagilia maji mti.
Mhifadhi misitu wa Wilaya ya Shinyanga kutoka taasisi ya Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Bwana Fabian Balele akipanda mti katika eneo la Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga ambapo miti hiyo imeandaliwa na taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la utamaduni wa Msukuma.
Hakimu mkazi mfawidhi Mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini Charles Machuwde akipanda mti ambapo miti hiyo imeandaliwa na taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la utamaduni wa Msukuma.
Hakimu mkazi mfawidhi Mahakama ya mwanzo Shinyanga mjini Charles Machuwde akimwagilia maji mti ambapo miti hiyo imeandaliwa na taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la utamaduni wa Msukuma.
Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) akizungumza baada ya shughuli ya upandaji miti katika eneo la Mahakama ya mwanzo iliyopo Nguzonane mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya tamasha la utamaduni wa Msukuma.
Hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Shinyanga Yusuph Zahoro akimpongeza Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) kwa kupaka rangi jengo la ofisi ya Mahakama ya mwanzo iliyopo Nguzonane kata ya Kambarage mjini Shinyanga.
Hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Shinyanga Yusuph Zahoro akimpongeza Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) kwa kupaka rangi jengo la ofisi ya Mahakama ya mwanzo iliyopo Nguzonane kata ya Kambarage mjini Shinyanga.
Mkuu wa kitengo cha maliasili na hifadhi ya mazingira Manispaa ya Shinyanga Bwana Ezra Manjerenga akiipongeza na kuahidi kuendelea kushirikiana na taasisi ya BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION.
Mhifadhi misitu wa Wilaya ya Shinyanga kutoka taasisi ya Wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Bwana Fabian Balele akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo naye amempongeza Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) kwa kupanda miti.
Hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Shinyanga Yusuph Zahoro na Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) wakiangalia mwonekano wa rangi katika jengo hilo.
Hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Shinyanga Yusuph Zahoro na Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) wakiangalia mwonekano wa rangi katika jengo hilo.
Hakimu mkazi mfawidhi Wilaya ya Shinyanga Yusuph Zahora akimshukuru Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK).
Mwonekano wa jengo la Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga tayari jengo hilo limepakwa rangi na taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK).
Mwonekano wa jengo la Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga tayari jengo hilo limepakwa rangi na taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK).
Mwonekano wa jengo la Mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga tayari jengo hilo limepakwa rangi na taasisi ya THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK).