LUDIMO ‘VIJANA MSIACHE KUSHIRIKI UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA’


Vijana nchini wametakiwa kujitokeza na kushiriki katika uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kuchagua viongozi wazuri na waadirifu watakaowaletea maendeleo kupitia uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani 

Rai hiyo imetolewa na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Nyamagana Ndugu Yusuph Ludimo wakati akihutubia wananchi wa kata ya Mkuyuni jijini Mwanza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mahakamani ambapo amewataka vijana kuacha kujitenga na michakato ya kisiasa pamoja na mawazo potofu ya kuamini kuwa kijana yeyote anaeshiriki uchaguzi na uboreshaji wa daftari la wapiga kura kuwa amepitwa na wakati kwa kuwa kufanya hivyo kutawaondolea fursa ya kuchagua viongozi wazuri wenye uwezo wa kuwatumikia na kuwaletea maendeleo

‘.. Wapo vijana wenzangu wakisikia masuala ya uboreshaji wa daftari wanaona hayawahusu, hawajitokezi, Mie nawaomba sana tusiache kujiandikisha na kushiriki uchaguzi kwa sababu hatuwezi kutengenisha maisha yetu na siasa, tunataka shule, zahanati, barabara, maji, umeme na maendeleo vyote hatuwezi kuvipata bila kushiriki uchaguzi na kujiandikisha katika daftari la wapiga kura ..’

Aidha Ndugu Ludimo amewataka wananchi wa kata hiyo kumshukuru na kumuombea kwa Mungu Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya reli ya kisasa SGR, vizimba vya ufugaji samaki na ujenzi wa meli inayowanufaisha moja kwa moja wananchi wa kata hiyo kwa kupata ajira, kupata huduma na kuongeza mzunguko wa fedha 
Kwa upande wake diwani wa kata ya Mkuyuni Mhe Donata Yusuph Gapi akafafanua kuwa kata yake imepokea fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa ya ghorofa shule ya sekondari mkuyuni na nyakurunduma, barabara ya mawe zahanati-nyakurunduma, ujenzi wa jengo la utawala mkuyuni sekondari, mikopo ya vijana, wanawake na watu wenye walemavu huku akiwaomba wananchi kuwaamini na kukichagua tena chama cha mapinduzi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 

Musa Magana ni Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi UVCCM wilaya ya Nyamagana ambae anaendelea na ziara ya kupandisha bendera za CCM kwa mabalozi wa wilaya hiyo, ambapo licha ya kuwashukuru vijana wa kata hiyo kwa kumchagua akaongeza kuwa anaridhishwa na kazi nzuri za maendeleo zilizofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu Hasan, Mbunge Mhe Stanslaus Mabula, Diwani na wenyeviti na kuwataka wananchi kuendelea kuwaunga mkono

 

Previous Post Next Post