Ticker

6/recent/ticker-posts

MAKALA: MAMBO MATATU MUHIMU UNAYOPASWA KUFANYA MARA BAADA YA KUFANYA USAILI WA AJIRA

 

Ili kuweza kushinda usaili wa ajira hatimaye kupata kazi uipendayo basi huna budi kuzingatia mambo muhimu ambayo nitakwenda kuyadadavua katika makala haya.

Makala hii ni maalumu sana kwako kwa sababu wengi wa watu wanaofanya usaili wa ajira wamekuwa hawazingatia mambo hayo. Wengi hudhani mara baada ya kufanyiwa usaili basi ni jukumu la ofisi au kampuni husika kumbusha kwamba amepata kazi kitu ambacho si kweli hata chembe.

Ila ukweli ambao unatakiwa kuuelewa mara baada ya kufanyiwa usaili wa ajira basi ni jukumu lako wewe kuwa makini na kufatilia mambo ambayo yatakusaidia kujenga ukaribu na ofisi husika hatimaye kupata kazi unayoitaraji.

Watu wengi wamekuwa wanaondoka mara moja  kuendelea na shughuli zao nyingine mara baada ya kufanyiwa usaili wa ajira. Kama na wewe ni miongoni mwa watu hao elewa kwamba unakuwa unakosea sana.

Hivyo leo nitakushikirisha mambo matutu unayopaswa kuyazingatia mara baada ya kufanyiwa usaili kama ifutavyo;

Uliza Kama kuna hatua nyingine ya usaili.

Kuna baadhi ya kampuni mfano mzuri baadhi ya maakampuni yale ya yakiserikari na yale yasiyo ya serikali hufanya usaili wa aina mbili yaani usaili kwa njia ya mahajiano na kwa njia ya kuandika. 

Hivyo ukijifanya wewe una haraka kuliko upesi na ukafanyiwa usaili wa aina moja pasipo kuhoji kama kuna aina nyingine ya usaili ni kwamba utakuwa unajikosesha mwenyewe  kazi husika.

Hivyo ushauri wangu kwako siku ya leo ni kwamba ni vyema ukahakikisha unahoji wahusika kama kutakuwa na  aina nyingine ya usaili ambayo itafanyika. Usiwe mnyonge kwani ni wajibu wako kuuliza kama kutakuwa na njia nyingine ya kafanyiwa asaili.

Andika barua ya shukrani 

Mara nyingi watu wengi huwa hatutambui nguvu ya shukrani. Mara baada kufanyiwa usaili jitahidi kuwa na nguvu ya shukrani kwa wale waliokufanyia usaili pale inapokubidi.

Mara tu baada ya usaili hakikisha kwamba unaandika maandishi mafupi kwa wake walikufanyia usaili. Andika maneno machache ya shukrani kwa fursa na thamani kubwa uliopewa na taasisi kuitwa katika usaili.

Uandishi huo ni lazima ufanyike ndani ya masaa 24. Maandishi hayo unaweza kutuma kwenye e-mail ya kampuni au kama utakosa uwezekano huo jitahidi ya kwamba unaandika katika karatasi.

Ukishamaliza kuandika katika karasi tafadhari usiweke karatsi hiyo katika bahasha kwani endapo utaweka katika bahasha itaonekana ya kwamba umetoa rushwa kwa yule aliyekufanyia usaili.

Kufatilia majibu ya usaili.

Kuonesha ya kwamba upo makini na kile unachokifanya hakikisha unafatilia majibu ya usaili ulioufanya kama umechaguliwa au laa. Hakikisha ya kwamba majibu hayo unafatilia ndani ya siku nne hadi tano. Usipige simu kama una uwezo wa kwenda nenda ukauulize na kama una upo mbali sana na eneo lile ndo utaweza ukapiga simu.  

Wakati mwingine unaweza kufatilia majibu yako kupitia chanzo umbacho kilitumika kukupa taarifa ya kuitwa kwenye usaili. Vitu kama magazeti, television, radio, email au anuani yako au ya kampuni husika huenda ndiyo kikawa chanzo cha kukupa habari ya majibu ya usaili wako.

Post a Comment

0 Comments