Na Mapuli Kitina Misalaba
Tamasha la utamaduni wa Msukuma (SHINYANGA SUKUMA
FESTIVAL SEASON 3, ambalo limeandaliwa na taasisi ya BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE
LIVE FOUNDATION” limeanza leo na litahitimishwa kesho Jumapili Juni 30, 2024
katika viwanja vya shule ya msingi Nhelegani kata ya Kizumbi Manispaa ya
Shinyanga.
Akizungumzia tamasha hilo Mkurugenzi wa BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE
LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) ameendelea kuwakaribisha wakazi
wa Mkoa wa Shinyanga na Mikoa jirani ikiwemo Mkoa wa Mwanza, Simiyu, Tabora
pamoja na Geita kujitokeza katika tamasha hilo.
MR. BLACK amesema kuwa malengo ya tamasha la
utamaduni wa Kisukuma ni kutunza na kuenzi utamaduni wa Msukuma pamoja na
kuendeleza umoja wa kabila hilo katika kushirikiana mambo mbalimbali yakiwemo
ya kijamii kwa lengo la kukuza uchumi.
Katika tamasha hilo yamefanyika maonyesho ya
Biashara, sanaa, ngoma za asili, burudani pamoja na Nyama choma” ambapo kauli
mbiu ya tamasha la utamaduni wa Msukuma kwa Mwaka huu 2024 inasema “UTAMADUNI
WETU URITHI WETU, SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA MAENDELEO YA TAIFA”
Viongozi na wananchi kutoka maeneo mbalimbali
wamejitokeza kushiriki katika tamasha hilo kama sehemu ya kuunga mkono
mwendelezo wa utamaduni wa kabila la Kisukuma “SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL SEASON
3, LEJIGUKULU LYA NZENGO”.
Misalaba Media imezungumza na baadhi ya wananchi
ambapo wamempongeza Mkurugenzi wa BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE
LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) kwa kuandaa tamasha hili ambapo
wameomba kuwa endelevu.
Wameeleza kuwa katika tamasha hili wamejifunza mambo
mbalimbali ikiwemo kuendelea kuenzi mila na desturi za kabila la Kisukuma ikiwemo
chakula mavazi, mavazi ya heshima pamoja na kilimo.
Naibu katibu mkuu wizara ya utamaduni, sanaa na
michezo Dkt. Suleiman Serera anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya kufunga
tamasha la utamaduni wa Msukuma kesho Jumapili Juni 30,2024.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI