Maswali ya msingi ya kujiuiliza kila wakati Ili kupata mafanikio

Mpenzi msomaji wa makala hii siku ya leo  tutangalia katika kujua umuhimu wa kufikiri ili kupata mafanikio. Mara kadhaa nimekuwa nikiandika ya kuwa watu wengi tumekuwa na maisha yalele ambayo yanatufanya tusisonge mbele kimafanikio hii ni kwa sababu tumekuwa tunafikiri mambo ya kawaida sana.

Pia kuna wakati mwingine hauhitaji nguvu nyingi katika kuyasaka mafanikio mafanikio yako, ila unahitaji akili za kufikiri ili kuyapata hayo mafanikio. Ukishapata hayo mafanikio ndipo unapohitaji nguvu nyingi katika kufanya kazi. Inawezakana ukawa hajaniekewa, ngoja nikueleweshe ni kwamba kila kitu kinaanza na kufikiri,  hapa ndipo wazo linapoanza kutengenezwa. Wazo hilo likishakamilika ndipo unapohitaji nguvu katika kufanya kazi.

Mambo ambayo unahitaji kujiuliza ili kupata mafanikio.

1. Unataka kuwa na nani?
Hili ni swali la muhimu sana la kujiuliza uwe msaka  mafanikio i. Mfano wewe ni mwanafunzi wakati unasoma katika masomo yako je umewahi kujiuliza unataka kuwa na nani katika maisha yako ya hapo baadae? pia na wewe mfanya biashara katika maisha yako umewahi kujiuliza unataka kuishi maisha gani? je biashara yako unataka iweje baada ya miaka kadhaa? je unataka kuwa unataka kuwa maarufu katika nyanja ipi ya kibiashar?

Ukishajiuliza maswali hayo lazima ujiuulize tena sifa hizo unazo au huna? na kama huna sifa hizo unazipata wapi. Ewe unayesoma makala haya shusha pumzi kisha twende sawa hebu jione upo  mahali fulani pale ambapo unataka kuwa  baada ya muda fulani ndoto zako zimetimia. Kimsingi ni kwamba endapo utayatafakari hayo na kuyapatia majibu sahihi   yanakupa hamasa ya kujua  malengo yako na jinsi ambavyo utaweza kuyatekeleza.

2.Unataka kutatua matatizo yapi?
Kwenye kutatua matatizo ndipo pesa zilipo. Unashangaa wala usishangae pia haujakosea kusoma. Ulimwengu wa leo ni ulimwengu wenye matatizo mengi ambayo yanahitaji majibu sahihi ya changamoto na mtoa majibu ni wewe. Unatoa macho ndio ni wewe mtoa majibu ya changamoto zinazowakabili watu. Badilisha mkao uliokaa kisha tuendelee,  tukiamungalia mtu ambaye aliyegundua mtandao wa facebook,  leo hii katatua tatizo la watu hasa katika nyanja ya mawasiliano kwa kutumia ubunifu wake kaamua  kutukutanisha watu pamoja na kuifanya dunia kuwa mtaa, huku tukiendelea kufurahia maisha hayo, mtu huyo leo ni miongoni mwa watu matajiri ulimweguni kwa sababu aliweza kusoma mazingira na kuona watu tuna changamoto na yeye akaja majibu ya changamoto .

Kutatua changamoto za watu hatuhitaji mifano kutoka kwa wazungu ila kila jambo unalotaka kulifanya kumbuka liwe linatoa majibu ya changamoto ya watu. Wewe unayefanya biashara ya kuuza chipsi endelea na kazi hiyo maana unasaaidia unatatua tatizo la njaa kwa haraka zaidi, kitu cha msingi ongeza ubunifu katika kazi yako ili kuongeza wateja wengi zaidi. Huo ni mfano tu ila kumbuka kutatutua matatizo ya watu ni njia sahihi ya   kupata pesa.


Na. Benson Chonya

Previous Post Next Post