MBUNGE wa Jimbo la Geita Mjini, Costantine Kanyasu imeipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kutoa fedha nyingi kuwezesha maendeleo ya eneo hilo.
Pongezi hizo zimetolewa hivi karibuni wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika wilaya hiyo kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo, Akizungumza katika Mkutano huo Maeneo ya mji mdogo wa katoro alisema Miradi Inatekelezwa na serikali
Alieleza kufurahishwa na mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa kwa sasa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami vilevile ujenzi wa hospitali ya Rufaa ya mkoa huo.
Kanyasu alisema kuwa utekekezaji wa miradi yote katika eneo hilo kwa kutumia fedha za serikali ni kwa mjibu wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo inatoa maelekezo kwa serikali yake.
Alitaja baadhi ya miradi ya ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana kuwa itawezesha watoto wa kike kusoma kwa juhudi na maarifa kwa kuwa jatika.mazingira rafiki ya kusomea.