MBUNGE KOKA AWAVUTIA MAJI YA DAWASA, JIKO LA GESI FAMILIA YENYE YENYE WALEMAVU WA NGOZI

Na Dismas Lyassa, Kibaha Mjini

MBUNGE wa Jimbo la Kibaha Mjini Mkoani Pwani ndugu Silyvestry Koka (pichani juu anayezungumza) amepongezwa kwa jitihada zake za kusaidia jamii na kuwa karibu na chama hicho wakati wote.

Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kibaha Mjini kilichofanyika leo, wajumbe wamempongeza Mbunge Koka, pamoja na mambo mengine kutokana na kusaidia familia yenye watoto wawili wenye ulemavu wa ngozi (albino) kwa kuwavutia maji ya DAWASA na kuwapatia jiko la gesi ili familia ipate muda wa kuwalinda watoto hao badala ya kwenda kuchota maji na kutafuta kuni.

“Mheshimiwa Mbunge ameguswa kwa kuimarisha ulinzi kwa familia zenye uhitaji maalum na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino). Siku zote Chama Cha Mapinduzi tunahitaji Amani na Utulivu,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.

Pichani anayesoma taarifa ni Katibu wa CCM Wilaya ya Kibaha Mjini ndugu Issack R.Kalleiya. Anayefuatia mwenye kiremba ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo Mwl Mwajuma Nyamka.

Taarifa imesisitiza kuwa, “Hatuwezi kudumisha Amani na Utulivu kama kuna baadhi ya raia wanaishi kwa hofu. Tunarudia kuliomba Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi wa raia na mali zao kwa kushirikiana na wananchi”.
Previous Post Next Post