MKANDARASI ATAKIWA KUHARAKISHA UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME WA JUA KISHAPU

 

Na Mapuli Kitina Misalaba

Kamishna wa Umeme Wizara ya Nishati Mhandisi Innocent Luoga ameridhishwa na hatua mbalimbali za maendeleo katika upatikanaji wa huduma ya Umeme Mkoa wa Shinyanga huku akimsisitiza mkandarasi katika mradi wa Umeme wa Jua Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mhandisi Luoga ameyasema hayo Juni 24,2024 baada ya kufanya ziara yake ya siku moja Mkoani Shinyanga ambapo ametembelea mradi wa Umeme wa Jua  katika Wilaya ya Kishapu pamoja na kituo cha kupoza na kusambaza Umeme Ibadakuli.

Pamoja na mambo mengine Mhandisi Luoga amempongeza meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga na menejimenti yake kwa usimamizi mzuri wa miradi ya Umeme huku akiwasisitiza wakandarasi kukamilisha kwa wakati miradi inayoendelea ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na serikali

 "Nikupongeze meneja kwa usimamizi kwa wakandarasi maana mkandasi ukimsimamia hawezi kuacha kufanya kazi mara nyingi sana wakandarasi wanazembea au wanakimbia ni kwa sababu tu haupo usimamizi mzuri kwahiyo mi nashauri tuhakikishe tunaongeza usimamizi kwa hao wakandarasi wetu ikiwa ni pamoja na kufanya nao vikao vya mara kwa mara ili kujua changamoto na maendeleo ya miradi”

“Yapo masuala ya usimamizi kwenye miundombinu na uharibufu unaofanyika ni wamaksudi au wengine kutokujua tu kwahiyo tuendelee kutoa elimu hasa kwa wananchi kuwaelezea madhara ya kuharibu miundombi ya Umeme wakati mwingine mnapanga ratiba kwenda kutoa elimu kwenye maeneo ambayo ni korofi zaidi”.

“Mradi wa Umeme wa Juan i muhimu sana mradi huu wa Kishapu ukija kukamilika maana yake wakati wa mchana tutakuwa tunatumia mradi wa Kishapu halafu wakati wa usiku hakuna Jua hakuna upepo tunawasha mitambo ya Maji na hii unakuwa mradi wa kwanza Tanzania wa kusalisha Umeme kwa kutumia Jua kwahiyo niwatake tu wakandarasi wa mradi huu wahakikishe wanamaliza mradi kwa wakati, kuchelewa chelewa kusiwepo na mradi huu ukamilike kwa kiwango kinachotakiwa”.amesema Mhandisi Luoga

APia Mhandisi Innocent akisoma amemhimiza mkandarasi wa Umeme wa Jua Kishapu kuhakikisha unatoa ajira kwa kuwapa kipaumbele wazawa.

Ataarifa ya miradi ya kusambaza Umeme kwa Mwaka wa fedha 2023\2024 meneja wa shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Leo Mwakatobe amesema mradi wa Umeme wa Jua unaotekelezwa katika maeneo ya Ngunga Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga umefikia asilimia kumi (10) ambapo unatarajiwa kukamilika Mwezi Februari 2025.

“Hali ya usambazaji Umeme imeendelea kuimarika kutokana na miradi mbalimbali ya kusambaza Umeme inayotekelezwa na TANESCO na ile ya kusambaza Umeme vijijini inayofadhiliwa na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA)”.

Pia meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga pamoja na mambo mengine amesema shirika hilo linasimamia miradi miwili (2) ya kimkakati ambayo ni mradi wa Umeme wa Jua Wilaya ya Kishapu pamoja na mradi wa kuboresha upatikanaji Umeme Bulyanhulu ikiwa lengo ni kuongeza uzalisha Umeme na kuboresha upatikanaji Umeme.

“Mradi wa Umeme wa Jua, kutokana na mahitaji ya Umeme kuongezeka serikali imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Umeme Jua maeneo ya Ngunga Kishapu ili kuongeza kiwango cha upatikanaji Umeme Mkoa wa Shinyanga na maeneo mengine ya Nchi, mradi huu unatarajiwa kuzalisha Umeme wa kiasi cha Megawati 150 ambapo mradi unathamani ya shilingi 323, 059,197, 768.30 na umegawanyika katika awamu mbili ya kwanza ni MW 50 na mkandarasi ni SINOHYDRO ambapo mkandarasi ameshakabidhiwa kazi na kuanza ujenzi Mwezi Oktoba 2023, kwa sasa mradi upo asilimia 10 na matarajio ya kukamilika ni baada ya Miezi kumi na nne (14).

“Mradi wa kuboresha upatikanaji Umeme uliopo eneo la Bulyanhulu, serikali kupitia shirika la Umeme kwa Mkoa wa Shinyanga kwa kuongeza mashineumba au Transfoma yenye ukumbwa wa 90\120MVA kwenye kituo cha kupoza Umeme wa grid cha Bulyanhulu 220\33kV mradi huu una thamani  ya dola za kimarekani 5,318,800.00 (bilioni 12) na mradi unatarajia kukamilika Septemba 2024”.amesema Mhandisi Mwakatobe

Kwa upande wake Mhandisi mwandamizi wa kampuni ya Sinohydro ameahidi kuzingatia maelekezo maelekezo ya Mhandisi Innocent Luoga ikiwa ni kukamilisha mradi kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa.

Naye Mhandisi wa mradi wa Umeme wa Jua Wilaya ya Kishapu Mhandisi Baraka Kanyika ameihakikishia serikali kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

TANESCO Mkoa wa Shinyanga inahudumia jumla ya Wilaya tatu ambazo ni Kahama, Kishapu na Shinyanga ambapo mpaka kufikia mwishoni mwa Mwezi Mei 2024 Mkoa unajumla ya watumiaji umeme 95, 206 na kwamba matumizi ya juu ya umeme yaliyofikiwa kwa Mwaka wa fedha 2023\2024 ni megawati 78.1.

Previous Post Next Post