Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akitoa maagizo kwa watendaji pamoja na wenyeviti wa vijiji na mitaa kusoma taarifa za mapato na matumizi kwenye maeneo yao.
Na
Mapuli Kitina Misalaba
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro amewataka
watendaji pamoja na wenyeviti wa vijiji na mitaa kusoma taarifa za mapato na
matumizi ili wananchi waweze kujua changamoto na mafanikio katika maeneo yao.
Ametoa agizo hilo wakati akisikiliza kero na
malalamiko mbalimbali katika mkutano wake wa hadhara kata ya Solwa Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga.
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Solwa pamoja na mambo
mengine wamesema ipo changamoto ya
mtendaji na mwenyekiti wa kijiji hicho kutosoma taarifa za mapato na
matumizi kwa muda mrefu.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro
ametumia nafasi hiyo kuwaagiza watendaji, wenyeviti wa vijiji na mitaa kusoma
taarifa za mapato na matumizi ili kuepusha mikanganyiko kwa wananchi hasa
katika miradi inayoendelea kutekelezwa kwenye maeneo yao.
DC Mtatiro pia amewasisitiza watumishi wote wa
serikali ambao wapo chini yake kutekeleza majuku yao kwa weledi kwa kuhakikisba
wanatoa huduma bora kwa wananchi.
“Sisi
tumepewa hizi kazi tumepewa na vifaa tunaofisi kila kitu tumepewa kazi yetu ni
kuwahudumia wananchi tunatakiwa kutoa huduma bora kwa wananchi ndiyo maana
nawaomba wasaidizi wangu watu wote wanaofanya kazi chini yangu kuanzia kwa
mkurugenzi mtendaji, watumishi wengine ambao wapo chini yake, magavana,
watendaji wa kata na watu wote wanaotoa huduma kwa wananchi huu wakati wangu
nikipata malalamiko yanayomhusu mtendaji yoyote wa dawati la serikali ambaye
hawahudumii wananchi ipasavyo moto wake ni mkubwa na moto utawaka kweli kweli”.amesema
DC Mtatiro
Katika mkutano huo wa hadhara wananchi wametaja kero
na malalamiko mbalimbali ikiwemo changamoto ya ukusanyaji wa ushuru wa mazao
pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara huku DC Mtatiro akimtaka mkurugenzi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga kushirikiana na wataalam wake katika
kutatua kero na changamoto zilizopo.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Shinyanga Stewart Makali amesema Halmashauri hiyo itaendelea
kushughulikia kwa uharaka changamoto zilizopo ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro
ameendelea na ziara zake kutembelea kila kata kwa lengo la kusikiliza na
kutatua kero na malalamiko mbalimbali ya wananchi ambapo amewasisitiza wananchi
kuwasiliana naye pale wanapobaini
changamoto kwenye maeneo yao ili iweze kutatuliwa kwa uharaka.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akizungumza
kwenye mkutano wake wa hadhara kata ya Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara kata ya Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Mkutano wa hadhara kata ya Solwa ukiendelea ambapo
lengo la mkutano huo ni mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatirokatika
kusikiliza na kutatua kero za wananchi.

Diwani wa kata ya Solwa Mhe. Awadhi Mbaraka Aboud
akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili
Julius Mtatirokatika kata hiyo.

Mkazi wa kata ya Solwa akitaja kero katika mkutano wa
hadhara wa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro.
Mkazi wa kata ya Solwa akitaja kero katika mkutano wa
hadhara wa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro.
Mkazi wa kata ya Solwa akitaja kero katika mkutano wa
hadhara wa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akitoa maagizo kwa watendaji pamoja na wenyeviti wa vijiji na mitaa kusoma taarifa za mapato na matumizi kwenye maeneo yao.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akitoa
maagizo kwa watendaji pamoja na wenyeviti wa vijiji na mitaa kusoma taarifa za
mapato na matumizi kwenye maeneo yao.
Mkutano wa hadhara kata ya Solwa ukiendelea ambapo
lengo la mkutano huo ni mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatirokatika
kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Stewart Makali naye akitolea ufafanuzi kero na malalamiko mbalimbali yaliyotajwa
na wakazi wa kata ya Solwa katika mkutano wa hadhara wa mkuu wa Wilaya ya Shinyanga
wakili Julius Mtatiro.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akitolea
ufafanuzi kero na malalamiko mbalimbali yaliyotajwa na wakazi wa kata ya Solwa
katika mkutano wake wa hadhara.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga wakili Julius Mtatiro akitolea ufafanuzi kero na malalamiko mbalimbali yaliyotajwa na wakazi wa kata ya Solwa katika mkutano wake wa hadhara.