MNEC MANGUZO ACHANGIA MILIONI TANO MKOA WA PWANI


Mjumbe wa Halmashuri Kuu ya Ccm ya Taifa Mhe.Qwihaya (Manguzo) ameshiriki katika Tafrija ya Chakula cha jioni iliyoambatana na Harambee ya kuchangia ujenzi wa Jengo la Ccm Mkoa wa Pwani ambapo mgeni rasmi alikua Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati kuu ya Ccm Mhe.Dr.Philip Isdor Mpango.
Mnec Manguzo alichangia jumla ya Tsh milioni tano (5,000,000) katika harambee hiyo ikiwa ni ishara ya kuunga mkono maendeleo ya Chama cha Mapinduzi katika Mkoa wa Pwani.



Previous Post Next Post