MR. BLACK APATA BARAKA ZA WAZEE KUELEKEA SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL SEASON 3

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mkurugenzi wa THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION Bwana Peter Frank (MR. BLACK) ambaye ndiye muandaaji wa  Tamasha la utamaduni wa Msukuma ameshiriki kupata baraka  za wazee katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga.

Pamoja na mambo mengine MR. BLACK amepata wasaha wa kunywa nao pombe ya kienyeji ya kisukuma na kucheza nao mchezo wa bao la kete ikiwa ni kuenzi Tamaduni ya Msukuma katima michezo, asili na pombe asili.

Wazee wamemshukuru MR. BLACK kwa kuwa na uthubutu katika kuchochea maendeleo kwa wakazi wa Nhelegani ambapo pia wamepongeza  juhudi na ubora  wa Tamasha hilo pia wameshauri mambo mbalimbali huku wakiomba Tamasha hilo liwe endelevu.

Ikumbukwe kwamba muandaaji wa Tamasha la utamaduni wa Msukuma  ametokea katika familia ya wauza pombe za kienyeji kapata elimu kupitia kipato cha uuzaji wa pombe za kienyeji, "Jasiri haachi asili" nah ii ndiyo sababu kuwa inayopelekea  kuendelea kuenzi mila na tamaduni za eneo hilo.

KUELEKEA TAMASHA LA UTAMADUNI WA MSUKUMA SHINYANGA, TAASISI YA THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION YAFANIKISHA MAREKEBISHO YA KUPAKA RANGI JENGO LA OFISI YA MAHAKAMA YA MWANZO MJINI SHINYANGA.

Tamasha la utamaduni wa Msukuma (SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL SEASON 3, ambalo limeandaliwa na THE BSL INVESTMENT COMPANY LIMITED AND THE TRUE LIVE FOUNDATION” Mwaka huu 2024 litafanyika kwa siku mbili kuanzia Jumamosi Juni 29 hadi Jumapili Juni 30 katika viwanja vya shule ya msingi Nhelegani kata ya Kizumbi Manispaa ya Shinyanga na kwamba hakuna kiingilio  “SHINYANGA SUKUMA FESTIVAL SEASON 3, LEJIGUKULU LYA NZENGO”.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika siku ya kufungua tamasha la utamaduni wa Msukuma Jumamosi Juni 29,2024.

Naibu katibu mkuu wizara ya utamaduni, sanaa na michezo Dkt. Suleiman Serera anatarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya kufunga tamasha la utamaduni wa Msukuma Jumapili Juni 30,2024.

Katika tamasha hilo yatafanyika maonyesho ya Biashara, sanaa, ngoma za asili, burudani pamoja na Nyama choma” ambapo kauli mbiu ya tamasha la utamaduni wa Msukuma kwa Mwaka huu 2024 inasema “UTAMADUNI WETU URITHI WETU, SHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KWA MAENDELEO YA TAIFA”

Tamasha hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, taasisi binafasi, vyama, wadau pamoja na wananchi ambapo pia wageni kutoka ndani na nje ya Tanzania watakuwepo.

MR. BLACK akizungumza na wazee baada ya kuwasili Nhelegani

 

Previous Post Next Post