Ticker

6/recent/ticker-posts

MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA NYAMAGANA AMEWATAKA WATANZANIA KUTUMIA VIZURI MITANDAO YA JAMII


Na Neema Kandoro Mwanza

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Nyamagana Peter Bega amesema hivi kumeibuka baadhi ya watu wakitumia mtandao wa X zamani twitter kutukana na kutaka kusambaza picha zisizo na maadili hivyo kushauri kufungwa.

Alisema endapo kutaendelea  kuwepo kwa habari zenye kuleta taharuki hapa nchini zitafifisha amani ya nchi ambayo imedumu kwa muda mrefu na hivyo kusababisha taifa kushindwa kudumisha mushikamano wake uliodumu muda mrefu hapa nchini.

"Hivi karibuni Mkurugenzi wa mtandao wa X zamani twitter  amesikika akisema kuwa ipo haja ya kuwekwa kwa maudhui ya habari zote na zile ambazo zinaendeleza mmomonyoko wa maadili ambazo ni kinyume na utamaduni wetu hivyo hakuna haja ya kuendelea kutazama mtandao huo ni bora tufunge" alisema Bega.

Bega aliipongeza kazi kubwa inayofanywa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) ya kuunganisha waumini wa dini hiyo na kuwa misingi mizuri ya kuimarisha umoja na mshikamano hapa nchini.

Alisema taasisi za dini zimefanya kazi kubwa muda wote nyakati ambapo zimetokea changamoto za magonjwa hapa nchini kwa njia za maombi na kuwezesha taifa kuondokana nazo kwa haraka.















Post a Comment

0 Comments