Mwenyekiti wa Jumuiya ya kupinga ukatili inayoitwa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Shujaa Sospeter Mosewe Bulugu, ameunga mkono juhudi za serikali katika kutokomeza Madada pa na Makaka poa nchini.
"Ninaungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, RC Chalamila kwa Kuwakemea Vikali wanaosema Madada Poa na Makaka Poa Wanadhalilishwa ama Kunyang'anywa haki zao. Hakuna aliyewadhalilisha bali, Wamejidhalilisha wenyewe na haki yoyote inayohatarisha kesho yetu haifai kutazamwa kama haki tena".
"Kama ni nguo zisizofaa Walijivika wenyewe, na hatua hizo ziendelee Kuchukuliwa, Hatuwezi Kuwatetea Watu wazima walioshindwa Kujitambua kwa Kuchagua kazi na Vitendo Vinavyohatarisha Kesho ya Watoto wa Afrika na hasa Tanzania ambao Leo hawajui jema na baya, Wataiga ama Kurithi nini Ikiwa wazazi watachagua kazi ya Kuuza Miili kisa Maisha,?".
"Haiwezekani Kubariki Vitendo hivi viovu, na Kama tumedhamiria kulinda Maadili yetu, basi tutambue anachokifanya Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe Hassan Bomboko ni Kupambana na Mlango au Chanzo kimojawapo cha Mmomonyoko wa Maadili".
"Nitumie fursa hii Kumuuliza kila anayedhani anawatetea wenye haki, kwamba unapata Hisia gani Ikiwa Wazazi wako wangechagua Kuuza Mili yao hiyo kama biashara ya Kukulea wewe? Vita hii ni Lazima tuitazame kwa Picha yenye Uhalisia."
"Tuache Ushabiki wa Kipumbavu na Umasikini wa Mawazo ama Kifikra, tuiache serikali ilinde hatma ya Vizazi vyetu."