WANANCHI mkoa wa Kilimanjaro wamejitokeza katika kuuaga mwili aliyekuwa Dereva wa Katibu Tawala mkoa Kilimanjaro Dk.Tixson Nzunda, Alphonce Edson (54)nyumbani kwake katika kijiji cha majengo mampya, kata ya Kahe wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Watu hao walipa ajali June 18 mwaka huu katika eneo la njiapanda ya uwanja wa Mataifa (KIA) wakieleka kumpokea makamu wa rais Dk Philip Mpango aliyekuwa akienda jijini Arusha kwa majukumu ya kikazi.
Akitoa salama za Rambirambi, mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu alisema wao kama mkoa wamepata pigo kubwa na itawachukua muda kukaa sawa kutokana na uhitaji wa watu hao katika ofsi hiyo.
Alisema marehemu Alphonce alikuwa mtulivu, mchapakazi na hajawai kuwa na ugomvi wala hana manunguniko wakati wote hata anapongwa kazi za ziada bila malipo.
"Hapana duniani tunapita, hakuna haja ya kuwa wababe. Watumishi wa ofsi yangu igeni mfano wa Alphonce, marehemu aliwai kuniendesha, ameendesha familia yangu, sijawai kusikia analalamika, huwezi kujua ni wakati gani amekasirika au amefurahi kupitiliza, hakika alikuwa ni mtu wa ajabu sana hapa tunajambo la kujifunza, "alisema RC Babu
Alisema kuwa, kifo chake ni pigo kubwa kwa ofisi ya mkuu wa mkoa alikuwa ni Dereva mwenye busara na hekima katika kazi
Aidha Mkuu huyo wa mkoa alitumia pia msiba huo kuwasihi wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro kuendeleza mshikamano uliopo na kuacha kuiga mambo ya watu wengine kwani hayaweza kuwasaidia.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi alisema kuwa yapo mambo ambayo tunapaswa kujifunza kupitia kifo cha Alphonce kuwa wema na waaminifu katika majukumu ya kila siku.
Alisema kuwa, kazi ya Mungu haina makosa na kuwataka kila mmoja kujiandaa maana hakuna ajuaye siku yake ya mwisho itakuwaje.
"Yapo mambo mema yaliyofanywa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kupitia misiba hii ambapo chama kinamshuku kwa jinsi alivyojitoa kupia misaba hii,"
Aidha amewataka viongozi kuhakikisha wanapambana kuhakikisha barabara ya kuelekea Mabogini Kahe Chekereni inakarabatiwa ili kupitika wakati wote ambapo jambo hilo litakuwa ni la kumuenzi marehemu Alphonce Edson.
Adha , Mkuu wa wilaya ya Moshi, Zephania Sumaye alitoa pole kwa familia kwa kuondokewa na mmoja wa familia ambaye alikuwa nguzo muhimu.
Alisema kuwa, hapa dunia hakuna kinachotokea ambacho hakijaruhusiwa na Mwenyezi Mungu na kuwataka familia kuendelea kufarijika kwa kutumia maneno ya biblia.
Alisema serikali itaendelea kushirikiana na familia pale pote watakapohitaji msaada kutoka kwa Serikali ya wilaya.
Akitoa salama kwa niaba ya Chama cha madereva wa Serikali Tanzania, Venus Ngalu alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha Alphonce Edson akiwa katika majukumu yake na aliyekuwa Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro.
Naye Mwakilishi wa Madereva wa Makatibu Tawala mikoa, Dereva wa Katibu Tawala mkoa wa Tabora,Kennedy Nangawe alisema kuwa Marehemu alikuwa akionyesha ushirikiano mkubwa katika Chama chao ambapo ni pigo kubwa kwa chama.
Akitoa mahubiri mchungaji wa kanisq la kiinjili kilteri (KKKT) Usharika wa Lowiri Mchungaji Thibias Msweka aliwataka waamini kujitadhimini mambo wanayofanya hasa katika maeneo wanayoishi hasa kwa wahitaji ili yawe alama pale wanapoondoka.
"Leo tujitafakari mimi na wewe tukiondoka utakumbukwa kwa lipi? Watumishi, angalieni msije mkakumbukwa kwa kuwa mzigo kwenye ofsi za watu.Leo watu wengi wanaishi kwa kiburi,majigambo na kunyanyua mabega.
Dunia ya sasa hakuna huruma na badala yake ni ukatili katika jamii, hatuwaonei huruma hadi kuamini kuwa wanapopata viungo vya binadamu wanapata utajiri.. huo ni uongo na naomba niwahakikishie utajiri hauji bila kufanya kazi."alisema Mchungaji
Aidha alimuomba mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro kuhakikisha kusimamia watu wenye ulemavu(Albino) huku akisisitiza kuwa watu hao wanawindwa sana.
Marehemu ameacha mjane na watoto sita na wajukuu wawili.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Nurdin Babu akitoa salama za mwisho