Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwenyekiti wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi ameeleza
kuwa hakuna mgogoro baina ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman
Mbowe pamoja na Makamu Mwenyekiti Tundu Lissu.
Ntobi ameyasema hayo Juni 15,2024 kwenye mkutano wake wa hadhara
katika kata ya Maganzo jimbo la Kishapu ambapo amesema kuwa baadhi ya watu wamekuwa na
sintofahamu na kudhani kuwa kuna mgogoro ndani ya CHADEMA baina ya Mwenyekiti
Mbowe pamoja na Lissu.
Mwenyekiti huyo wa CHADEMA
Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi amewatoa hofu watanzania kuwa hakuna
mgogoro ndani ya CHADEMA huku akihimiza kuendelea kukiunga mkono chama hicho katika
utetezi wa haki za wananchi.
“Chama chetu cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA katika
Tanzania hii hakina mgogoro wowote, hatuna mgogoro baini ya Mhe. Lissu wala
hakuna mgogoro baini ya Mhe. Lissu na Mhe. Mbowe wote hawa ni majembe ni kitu
kimoja Chama chetu kuna mtu tu mmoja hakushinda uchaguzi mmoja akaingiza
mgogoro wa kwake binafsi, jambo hilo nimekuwa naulizwa nimeona ni vema
niwaambie na watu wa Maganzo maana CCM wamechukua kama Propaganda ya kusema
CHADEMA imesambaa CHADEMA itabomoka hiki chama hakitabomoka kwa sababu CHADEMA
ni mpango wa Mungu”.amesema Ntobi
Katika hatua nyingine
Ntobi amemsisitiza mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringa Macha kushughulikia
changamoto za jeshi la jadi Sungusungu kuwa baadhi ya watu katika jeshi hilo
hutajwa kukamata na kutishia wananchi.
“Nimtumie salamu mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringa
Macha nataka nimwambie tabia ya Sungusungu iliokisiri katika jimbo la Kishapu
kukamata, kutishia watu kukusanya michango hii tabia tutamshitaki yeye na hao
Sungusungu wake ni mapema nampa tamko akome”.
“Sungusungu hawapo kwenye sheria yoyote ya nchi ni wanafanya kazi kihuni tu na wamelelewa
kihuni na chama cha mapinduzi kuwatisha watu wanaotetea haki hakuna sheria
yoyote ya Sungusungu katika taifa hili na ninyi watu wa Maganzo na vijiji
vingine kakataeni na muwashughulikie, nimeambiwa kuwa baadhi ya Sungusungu walikwisha
kuwapeleka Mahakamani wao kama wao sasa mimi namtumia salamu mwenyekiti wa
ulinzi na usalama wa Mkoa wa Shinyanga jambo hili halipo Kishapu tu lipo Solwa,
lipo Ushetu, lipo Shinyanga mjini kwenye kata ya Kolandoto hawa Sungusungu
wakome kabisa kuwanyanyasa wananchi”.amesema Ntobi
Wakati huo huo Mwenyekiti
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel
Ntobi ameitaka serikali kushusha bei za mafuta ya Petroli ambapo amesema hatua
hiyo itasaidia kurahisisha usafirishaji wa bidhaa mbalimbali hapa nchini.
Pia Ntobi amewahimiza
wananchi wa jimbo la Kishapu na Mkoa wa Shinyanga kwa ujumla kujitokeza kwa
wingi wakati wa zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la makazi pamoja na
daftari la kuduma la wapiga kura ili kushiriki vema katika uchaguzi wa serikali
za mitaa Mwaka huu 2024 pamoja na uchaguzi mkuu Mwaka 2025.
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel Ntobi akizungumza na wananchi kwenye mkutano wake wa hadhara katika kata ya Maganzo jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga.

Wananchi wa kata ya
Maganzo jimbo la Kishapu wakiwa katika mkutano wa hadhara ambao umeandaliwa na Mwenyekiti
wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Mhe. Emmanuel
Ntobi.