PROF.MKENDA AITAKA TCU KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA VYUO VYA ELIMU YA JUU NCHINI






WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa majadiliano kati ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Vyuo Vikuu nchini kuhusu utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023,Mkutano uliofanyika Juni 7,2024 jijini Dodoma.


WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akisisitiza jambo wakati akifungua Mkutano wa majadiliano kati ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Vyuo Vikuu nchini kuhusu utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023,Mkutano uliofanyika Juni 7,2024 jijini Dodoma.



Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Prof. Charles Kihampa,akielezea lengo la Mkutano wa majadiliano kati ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Vyuo Vikuu nchini kuhusu utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023,Mkutano uliofanyika Juni 7,2024 jijini Dodoma.



BAADHI ya washiriki wakimsikiliza Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,(hayupo pichani) wakati akifungua Mkutano wa majadiliano kati ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) na Vyuo Vikuu nchini kuhusu utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023,Mkutano uliofanyika Juni 7,2024 jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ameitaka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuendelea kushirikiana na Vyuo vya Elimu ya Juu nchini katika mchakato wa kufanya maboresho ya mitaala ili iendane na Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mitaala Mipya ya ElimuMsingi

Prof. Mkenda amesema hayo jana Jijini hapa wakati akifungua Mkutano wa majadiliano kati ya Tume hiyo na Vyuo Vikuu nchini kuhusu utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 ambapo amewaomba Viongozi hao wa Vyuo Vikuu kutoa mrejesho pale wanapoona kuna lolote lenye changamoto ili ifanyiwe kazi katika kuhakikisha utekelezaji unafanyika kama unavyotarajiwa

Ameongeza kuwa majadiliano kati ya Tume hiyo na Vyuo Vikuu ni muhimu pamoja na kwamba TCU inaweza kutoa maelekezo lakini ni muhimu yafanyike kupitia majadiliano ili kuwa na ushirikishwaji wa wadau wa elimu ya juu.

“Mageuzi ya mitaala yanagusa ngazi zote za elimu kwa watu wanapohoji juu ya ubora wa elimu hawaangalii tu elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu bali wanagusa mpaka elimu ya juu” amesisitiza Prof. Mkenda

Prof.Mkenda ameongeza kuwa katika kutekeleza mageuzi ya elimu katika ngazi ya chini, vyuo vikuu vinapaswa kujipanga katika kuandaa walimu wanaokwenda kufundisha katika shule za Sekondari, hivyo ni lazima kuangalia nini sera inahitaji.

Waziri Mkenda amesema pia katika sera na mitaala iliyoboreshwa kuna masomo mapya ambayo yanahitaji walimu akitolea mfano somo la ujasiriamali ambalo halina walimu wa kutosha na kupelekea utekelezaji wa Sera mpya katika elimu ya Sekondari kuanza na Mkondo wa Amali pekee.

Aidha, amewataka Viongozi hao wa Elimu ya Juu kuanza kujiandaa kupokea wanafunzi walisoma kidato cha tano katika mkondo wa elimu amali ambao watakuwa na Dipmola watakaohitaji kujiunga na shahada za amali katika fani mbalimbali.

Kwa upande wake Katibu Mtendaji Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Prof. Charles Kihampa amesema kuwa kikao hicho kitajadili juu ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mitaala mipya ya elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu na namna Vyuo Vikuu vitakavyoboresha Mitaala ili kuendana na mabadiliko haya na kuzalisha wanafunzi wenye ujuzi watakao weza kujiajiri ama kuajiriwa

“Dhumuni kubwa la kikao hicho ni kuanzisha Rasmi mchakato wa mabadiliko ya mtaala wa vyuo vikuu kwa lengo la kukamilisha mnyororo wa Elimu kuanzia Elimu ya msingi hadi Elimu ya juu”amesema Prof.Kihampa
Previous Post Next Post