QWIHAYA AHITIMISHA ZIARA NYAMAGANA KWA KUCHANGIA MIFUKO 720 YA SARUJI


Na Neema Kandoro Mwanza

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (Ccm), Leonard Qwihaya Maarufu kama Manguzo Leo 27/6/ 2024  amehitimisha ziara yake ya siku Tatu kwenye Jimbo la Nyamagana kwa kutoa Msaada wa Mifuko ya saruji 720 Kwa ajili kitumiwa katika ujenzi wa ofisi za chama hicho.

Qwihaya amewataka wapenzi na wakereketwa wa chama hicho kuwa mstari wa mbele katika Ujenzi wa ofisi Ili waweze kuwa na uhakika wa sehemu ya kufanyia kazi zao za Kila siku.

Alisema Ujenzi wa miundombinu ni hatua njema katika kuimarisha uhai wa chama na hivyo kuendelea kuwa kimbilio la watanzania muda wote.

Katika Ziara hiyo vilevile amewataka Watanzania wote waliokaribu kufikisha umri wa Miaka 18 kuwa tayari kujiandikisha kwenye Daftari la makazi na like la wapiga kura Ili ukifika muda wa Uchaguzi watumie kuchagua viongozi wanaowataka.

Qwihaya Maarufu kama Manguzo amewashukuru wanachama wa chama hicho kwa kujitolea kuchangia kwa hiari yao wenyewe katika kipindi Ujenzi wa ofisi za chama Ili waweze kuwa na nyumba za uhakika ambazo vilevile wataweza kupangisha na chama hicho kujiongezea kipato.









Previous Post Next Post