QWIHAYA ATAKA WANA CCM KUCHANGIA MAENDELEO YA CHAMA


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Leonard Qwihaya amewaomba wakereketwa na wapenzi wa Chama hicho kujitolea katika kukijenga Chama hicho kwa kukitolea misaada ya fedha na nguvu kazi Ili kuendelea kuongoza taifa.

Wito huo ameutoa Leo katika maeneo tofauti katika Kata ya Pamba, Igogo, Mkuyuni, Butimba na Nyegezi alipokabidhi mifuko 200 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Chama Ngazi ya Kata ambapo kila kata ilipata Mifuko 40.

Alisema ujenzi wa chama ni jukumu la wanachama wenyewe hivyo wanalo jukumu la kuchangia katika maendeleo ya eneo hilo kwa kutoa vitu mbalimbali ama kujitolea kwa nguvu kazi.

Qwihaya alisema anatekeleza wito aliutoa kwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Staslaus Mabula Mwezi Disemba Mwaka Jana wa kuchangia mifuko ya saruji kwa kila kata kwenye jimbo hilo.

Hamasa iliyoanzishwa na MNEC huyo imewezesha Kata ya Nyegezi Kuchanga zaidi ya shilingi milioni saba za papo kwa papo kwa ajili ya ujenzi na ununuzi wa ardhi.









Previous Post Next Post