RAS MKOA WA LINDI BI. ZUWENA OMARY WATENDAJI WA HALMASHAURI FANYENI UFUATILIAJI NA KUCHUKUA HATUA KUFUTA HOJA ZA CAG

 

Na,Elizabeth Msagula,Lindi


Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Bi. Zuwena Omary amewataka watendaji kufanya ufuatiliaji na kuchukua hatua za hoja za Mkaguzi na mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kuepuka kujirudia rudia na kuwa nyingi .

Ametoa rai hiyo  Juni 25, 2024 Wilayani Nachingwea katika kikao cha baraza Maalumu la kisheria kuhusu kupitia na kujadili taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali .

''Kinachosababisha kujirudia rudia kwa hoja ni kutofanya vya kutosha na kimsingi kinachotupelekea hoja ni sisi wenyewe kuchelewa kufanya maamuzi....ni ufuatiliaji wetu tu " Zuwena Omari Katibu Tawala Lindi.

Aidha, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya hiyo kwa kupunguza hoja 7 za CAG kutoka kwenye hoja 17 na mwelekeo wa kufuta hoja 5.

Katika hatua nyingine,ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kuona umuhimu wa kushiriki zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ambalo linatarajiwa kuanza siku chache zijazo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nachingwea Adinani Mpyagila amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Telack kwa namna anavyoendelea kuwahudumia wananchi wa mkoa huo katika kutatua changamoto mbalimbali.

" Tumeona namna ambavyo Mkuu wa Mkoa alivyopambana katika kutatua changamoto za wananchi hasa kipindi kile cha mvua nyingi kilichopelekea kuaribika kwa miundombinu hasa ya barabara , amefanyakazi kubwa mnao'' Mhe. Mpyagila.

Na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nachingwea amesema Halmahauri ya Nachingwea itazingatia yote ili iendelee kufanya vizuri kwa kupata hati safi kama ambavyo imeendelea kupata miaka sita mfululizo.




Previous Post Next Post