Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akisoma taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro katika kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Serikali itaendelea kuboresha huduma za kijamii
ikiwemo upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo yote ya kata 17 za Manispaa ya Shinyanga.
Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya
Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko wakati akisoma taarifa ya Mkuu wa Wilaya ya
Shinyanga Wakili Julius Mtatiro katika kilele cha maadhimisho ya kupinga
ukatili dhidi ya wazee ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.
Amesema itaendelea na uboreshaji wa huduma za
kijamii ikiwemo kutoa elimu bila malipo na kuboresha upatikanaji wa huduma za
afya katika maeneo mbalimbali ili kuepusha
usumbufu unaojitokeza kwa wazee kutembea ubali mrefu kufuata huduma hizo.
“Tutaendelea
na uboreshaji wa huduma za kijamii ikiwemo kutoa elimu bila malipo na kuboresha
upatikanaji wa huduma za afya katika maeneo yetu ili wazee wetu wasitembee
umbali mrefu kupata huduma hizo kama mnavyoona katika serikali yetu ya awamu ya
sita imeendelea kujenga na kuboreshaji huduma za kutolea huduma za afya ambapo
karibia kata zote katika Halmashauri yetu zinavituo vya kutolea huduma za afya”
“Nimtake
mganga mkuu wa Wilaya ya Shinyanga kwa
kushirikiana na wizara za TAMISEMI na wizara ya Afya kuimarisha upatikanaji wa
dawa na wataalam wabobezi wa magonjwa ya wazee hususan kwenye Hospitali zetu za
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na kuhakikisha kundi hili muhimu
linatambuliwa na kupewa kapaumbele ikiwa ni pamoja na kupatiwa vitambulisho au
kadi za matibabu ya wazee”.
“Kuhusu
suala la tiba kwa wazee serikali imeunda kamati maalum kwa ajili ya kuleta
mapendekezo serikalini kuhusu namna ya kukabiliana na changamoto hii, wakati
serikal ikiendelea kupitia mapendekezo ya kamati hiyo nataka niwaahidi wazee
wangu kuwa yale yote yanayowafanya wazee kuwa kwenye kundi hatarishi tutayashughulikia”
“Kwa
ujumla changamoto na maombi yote mliyoyawasilisha niya msingi hivyo basi
serikali tumeyapokea na tutajitahidi kuyashughulikia na kwa bahati nzuri
masuala yote mliyoyaeleza yapo kwenye ilani yetu ya uchaguzi ya 2020\2025 na pia tumeyajumuisha
kwenye mpango wa tatu wa taifa wa maendeleo kwa Miaka mitano ambayo utekelezaji
wake tuliuanza Mwezi Julai 2021”.
Kupitia taarifa hiyo pia amewasisitiza wazee
kuendelea kuhimiza malezi bora kwa watoto pamoja na kudumisha amani na usalama ili
kuendelea kujenga taifa bora.
“Niwakumbushe
wazee kuendelea kuhimiza malezi bora kwa watoto ili kujenga taifa la watu
waandilifu, waaminifu, na wazalendo kwa nchi yao wasio jihusisha na vitendo
viovu vya wizi, rushwa, matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine ambavyo
ni kinyume cha maadili na tamaduni zetu “.
“Kama
mnavyofahamu amani na usalama ni msingi wa maendeleo bila ya amani hakuna maendeleo na zaidi pasipo na amani wenye
kuathirika zaidi ni pamoja na wazee hivyo wazee wangu tunalojukumu kubwa la
kuhakikisha tunadumisha amani katika Wilaya yetu”.
“Kapaumbele
kingine ni kulinda uhuru, muungano wetu na mshikamano mambo haya hayana mbadala
hivyo tutaendelea kuyaenzi, kuyatunza na kuyaendeleza pili kuendeleza jitihada
za kukuza uchumi na hapa tunaendeleza kazi nzuri ikiwemo ujenzi wa miundombinu
ya usafiri na huduma za usafirishaji lengo ikiwa ni kuchochea ukuaji wa uchumi
nchini”.
Awali akisoma risala, mwenyekiti wa baraza la
ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano amesema baraza hilo
linaendelea kukemea kila aina ya ukatili kwa wazee ikiwemo ukatili wa
kutelekezwa na familia zao.
“Ukatili
kwa wazee upo katika maeneo mengi ikiwa ni pamoja na mauaji ya vikongwe,
kutelekezwa wazee na familia, kunyimwa fursa ya maendeleo ya kiuchumi na
kutoheshimiwa wazee kwenye nafasi za huduma mbalimbali tamko letu sisi wazee
sehemu zote za kutolea huduma ni mzee kwanza jambo la pili waganga na wauguzi wanajitahidi
kuwapa huduma wazee wetu kwa kidogo kinachopatikana”.amesema
mzee Tano
Kwa upande wake mganga mkuu wa Wilaya ya Shinyanga
Dkt. Elisha Robert amesema tayari ipo ratiba ya wataalam wa afya kupita kila
kata kwa ajili ya zoezi la upimaji ili kutambua hali za afya kwa wazee.
“Tutakuwa
na ratiba ya kupita kila kata angalau kila Mwezi mara moja tutakuwa tunaifikia
kata moja kwa ajili ya kuwafikia wazee wote walipo ili waweze kupata hizi
huduma ambazo zinaendelea hapa tunafanya hivo kwa sababu sasa hivi tatizo
linalowakumba wazee ni ugonjwa wa shinikizo la damu”.
“Ukienda
katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa tunapokea wagonjwa ambao wanakiharusi yaani ambao wanapoteza nguvu
sehemu moja ya mwili yaani mmoja wawili hadi wane ndani ya masaa 24 hii hali
inatokea kwa sababu wengi hatutambui afya zetu, tunatembea tunafanya kazi
lakini hatutambui afya zetu kwahiyo tukianza hii kampeni ya kupita kila kata
wazee wote watapata nafasi ya kutambua
afya zao na watakapokuwa wametambua afya zao sisi kwa upande wa idara ya afya kazi
yetu ni kuwahudumia wazee na ndiyo kipaumbele chetu”.amesema
Dkt. Elisha
Maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee kwa
Mwaka huu 2024 yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga na kwamba
yamehudhuriwa na wazee wenye umri kuanzia Miaka 60, viongozi mbalimbali wa
serikali, wadau pamoja na viongozi wa mabaraza ya wazee katika ngazi ya kijiji,
mtaa, kata na Manispaa ya Shinyanga.
Katika maadhimisho hayo shughuli mbalimbali
zimefanyika ikiwemo upimaji wa afya kwa wazee, utoaji wa elimu ya kujikinga
magonjwa yasiyoyakuambukiza pamoja na elimu ya kupambana na ukatili kwa wazee.
Katika huduma zilizotolewa juu ya magonjwa yasiyoyakuambukiza ni pamoja
na kupima presha, Sukari na magonjwa ya moyo pia wataalam wa afya wametoa
ushauri kwa wazee hao juu ya kuepukana na magonjwa yasiyoyakuambukiza pamoja na
namna ya kuishi kwa wale wenye matatizo hayo.
Lakini pia umetolewa ushauri nasaha juu ya lishe
bora kwa wazee ikiwa ni pamoja na matibabu sahihi na kujitokeza katika follo-
up kwa wenye matatizo hayo inayofanyika kila siku ya Alhamisi katika kituo cha
afya Kambarage.
Kilele cha maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ni kila Mwaka ifikapo Juni 15 ambapo kwa Mwaka huu 2024 katika Manispaa ya Shinyanga kauli mbiu inasema “WAZEE WA SHINYANGA TUPAZE SAUTI TUYADUMISHE MAADILI MEMA”
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano akisoma risala ya baraza hilo katika kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee Mwaka 2024.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano akikabidhi risala kwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee Mwaka 2024.
Mganga mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee Mwaka 2024 ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.
Mganga mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee Mwaka 2024 ambayo yamefanyika katika Zahanati ya Old Shinyanga.
Afisa ustawi wa jamii wa
Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Bi. Ansila Materu akizungumza
kwenye kilele cha maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wazee Mwaka 2024.
Maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili dhidi ya
wazee kwa Mwaka huu 2024 yakiendelea katika viwanja vya Zahanati ya Old
Shinyanga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.

Shughuli mbalimbali zikiendelea ikiwemo upimaji wa afya kwa wazee juu ya
magonjwa yasiyoyakuambukiza ambayo ni presha, Sukari na magonjwa ya moyo katika
Zahanati na Old Shinyanga.