SERIKALI YA FINLAND KUPITIA UNFPA YATOA MAFUNZO KWA WATEKELEZAJI MRADI WA CHAGUO LANGU, HAKI YANGU - KAHAMA





Serikali ya Finland Kupitia Shirika la UNFPA limetoa mafunzo kwa watekelezaji wa mradi ujulikanao kama 'Sauti yangu, Haki yangu' kwenye manispaa ya Kahama kujadili agenda mbalimbali hususa ni ushirikishwaji wa wanaume katika kupinga vitendo vya ukatili kwenye jamii.

Mafunzo hayo yamefanyika  Juni 07, 2024 katika moja ya ukumbi iliopo kanisa la Romani katoriki jimbo la kahama mkoani Shinyanga.

Mafunzo hayo yaliyo wakutanisha washiriki wanaotekeleza mradi wa 'Chaguo langu, haki yangu' (CLHY) kutoka katika kata 7 ambazo ni kata ya Kagongwa, Kilago, Nyasubi, Mhongolo, Majengo, Mhungule na Nyahanga ambao ni makundi ya wanaume, vijana, wazee, watendaji wa kata, maafisa maendeleo kata kutoka ndani ya manispaa hiyo.

Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo kiongozi kutoka Shirika lisilo la kiserikali nchini HelpAge Tanzania Bw. Joseph Mbasha amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo watekelezaji wa mradi huo ili waweze kutoa elimu kwenye jamii inayowazunguka na kufikia malengo waliyojiwekea.


"Mradi huu wa 'Chaguo langu, haki yangu' umefadhiriwa na serikali ya Finland kupitia UNFPA na kutekelezwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum pamoja na Wizara ya Afya ofisi ya Waziri Mkuu na mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo HelpAge Tanzania ambapo leo tumekutana na watekelezaji wa mradi huu hapa kahama tunaamini kama wanaume watashiriki ipasavyo katika uwajibikaji kwenue familia zao basi vitendo vya ukatili vitakwisha kwenye jamii kwasababu mwanaume ndio kichwa cha familia na mwenye ushawishi mkubwa kwenye jamii", amesema Joseph Mbasha.

"Lengo la mafunzo na mradi huu ni kuwafanya wanaume washiriki kutokomeza vitendo vya ukatili hasa vinavyowalenga wanawake na watoto na kuwafanya wanaume na vijana washiriki katika kutokomeza vitendo vya ukatili na unyanyasaji kwa wanawake, wasichana na wenye ulemavu ambapo kupitia walsha hii tuliokutana leo itasaidia kuwajenga na kuyawezesha kukutana na makundi mbalimbali ndani ya jamii wanayoishi  kwa kuwapa mbinu za kukabiliana na mila potofu kupitia elimu katika mabaraza ya wazee, mikusanyiko mbalimbali, nyumba za ibaada na jumuiya za vijana", ameongzeza Joseph Mbasha.

"Matarajio yetu ni kuwa na jamii yenye uelewa na inayoheshimu haki za makubdi tofauti katika jamii, kuwajengea uelewa na utayari wanaume na wavulana kushiriki katika kuzuia na kupambana na vitendo bya ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni na ukeketaji dhidi ya wanawaje na wasichana na kuhamasisha wanaume na wavulana kushiriki katika afya ya uzazi na malezi kama wazazi na walezi", ameongeza Joseph Mbasha.

Kwa upande wake Afisa ustawi wa jamii manispaa ya Kahama Abrahamani Nuru ameeleza zamila ya kuwahusishwa akina baba na vijana wa kiume katika mapambano dhidi ya ukatili.


"Ni vigumu kupata ushindi wakati nusu ya timu ipo nje ya uwanja, wanaume wengi walezi wakuu na wasimamizi wa mila na desturi hivyo tukihusisha makundi haya ni hakika tutaongeza nguvu ya mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili kwenye jamii zetu", amesema Abrahamani Nuru.

Kwa upande wake mratibu wa mafunzo hayo Bi. Swaiba Chemchem amebainisha jukumu la wanaume na wavulana katika kukuza usawa wa kijinsia na haki za kijanii.


"Jukumu la wanaume na wavulana katika kukuza usawa ni kubadili mitazamo kuhusu uwezo wa wanawake, kushiriki katika masuala ya uzazi na malezi ikiwa ni pamoja na kupanga uzazi na kushiriki huduma za afya ya uzazi, kushiriki katika utoaji elimu na taarifa za ukatili ili kuelewa madhara ya ukatili wa kijinsia na kushiriki kufichua na kutoa taarifa za matukio ya ukatili", amesema Swaiba Chemchem.


Kiongozi kutoka Shirika lisilo la kiserikali nchini HelpAge Tanzania Bw. Joseph Mbasha akizungumza wakati wa mafuzo hayo.


Afisa ustawi wa jamii manispaa ya Kahama Abrahamani Nuru akizungumza wakati wa mafunzo hayo.


Mratibu wa mafunzo hayo Bi. Swaiba Chemchem akizungumza wakati wa mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.



Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Majadiliano yakiendelea.



Mafunzo yakiendelea.

Mafunzo yakiendelea.

Majadiliano yakiendelea.


Majadiliano yakiendelea.

Mmoja wa washirikia akiwasilisha mchango wake wakati wa mafunzo hayo.

Mafunzo yakiendelea.








Majadiliano yakiendelea.

Majadiliano yakiendelea.

Picha ya pamoja.

Previous Post Next Post