Ticker

6/recent/ticker-posts

SHEIKH WA MKOA WA SHINYANGA ISMAIL MAKUSANYA ASISITIZA WAUMINI WA KIISLAM KUSHIRIKI KIKAMILIFU UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA UCHAGUZI MKUU

Sheikh  wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya amewataka waumini wa dini  ya  kiislamu  Mkoani Shinyanga na watanzania wote  kushiriki katika zoezi la uchaguzi  wa serikari za mitaa linalotalajiwa kufanyika baadaye Mwaka huu nchini kote .

 Akiongoza swala ya Iddi  El Adha  katika uwanja wa sabasaba mjini Shinyanga  Sheikh  Makusanya amewaomba waumini wa dini ya kiislamu na jamii nzima kushiriki kikamilifu katika uchaguzi  wa serikari za mitaa utakaofanyika mwaka huu  ili kutimia haki yao ya msingi  ya kuchagua na kuchaguliwa.

Pia ametoa wito kwa  waumini wa dini ya kiislamu  kuwa chachu  ya kulinda  na kudumisha amani iliyopo.

“Mwaka huu serikali yate pendwa, serikali yetu tukufu inafanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwahiyo ndugu zangu waislamu nakuombeni ushiriki sana katika chaguzi hizi tena tushiriki kwa ukamilifu wale ambao watakuwa wanatarajia kuomba nyazifa mbalimbali za uongozi katika mitaa yetu  wakiona fursa na vigezo wanavyo waombe lakini pia kwa wale ambao hawaombi nafasi yoyote usiache kushiriki katika jambo hili la uchaguzi katika mitaa yetu”.

“Mungu akijalia katika Mwaka ujao 2025 tutakuwa na uchaguzi mkuu kwahiyo nakuombeni waislamu tushiriki, tushiriki kwa amani na utulivu na sisi waislamu kila mtu anahiali ya kuwa katika chama chochote kilichoandikishwa kwa mujibu wa sheria kila mtu anahaki ya kuchagua chama ambacho yeye kinamridhia kwahiyo vyama vyetu visitufanye sisi tukavunja amani na utulivu kila mmoja anahaki ya kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu kwahiyo nakuombeni mshiriki katika zoezi”.amesema Sheikh Makusanya

Katika mawaidha yake  wakati wa swala ya Iddi El Adha Sheikh wa  Wilaya ya Shinyanaga  Soud Kategile amewaasa  waislamu  kuendelea kuwa wazalendo na kudumisha amani iliyopo sanjari na kulinda maadili ya Taifa la Tanzania

“Shukurani si kusema asante shukurani haiishii kusema Alhamdulillah peke yake lakini tumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia amani katika nchi yetu na tuilinde amani hii kwa sababu ni tunu kwetu ambayo wengi wanaitamani katika nchi za wenzetu bila ya amani sisi tusingekuwepo hapa amani haina dini, amani haina kiongozi amani haina mtawaliwa kwahiyo tumshukuru mwenyezi Mungu kwa kutujalia amani, ndugu zangu waislamu kila mmoja aondoke na jambo hili la kutunza amani katika nchi yetu”.amesema Sheikh Kategile

Wakiongea na Misalaba Media baadhi  ya waumini wa dini ya kiislamu   wemesema watazingatia mafundisho waliyopatiwa na viongozi wa dini  kupitia mawaidha kwenye ibada ya Eid El Adha ikiwemo kushiriki kikamilifu uchaguzi wa serikali za mitaa baadaye mwaka huu.

 

Sheikh  wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya akiongoza swala ya Iddi  El Adha  katika uwanja wa sabasaba Kambarage mjini Shinyanga  leo Jumatatu Juni 17,2024.

 

Post a Comment

0 Comments