Na MWANDISHI MAALUM
-Lagos, NIGERIA
KATIKA kuhakikisha fursa za Tanzania zinatangazwa
uptia diplomasia ya uchuni, Ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria, umeendesha
jukwaa la kuvutia uwezaji nchini Nigeria.
Majukwaa hayo ambayo yamefanyika juzi na jana katika
majimbo ya Enugu na Lagos kwa lengo la kjua mkakati wa uwekezaji nchini
Tanzania ambapo ilizishirikisha makampuni yenye uwezo wa kuwekeza nje ya
Nigeria.
Aidha, Ubalozi ulishirikiana na Kituo cha Uwekeaji
Tanzania (TIC), na kuwakilishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,
Dkt. Binilith Mahenge na Afisa Uwekezaji Mwanadamizi wa TIC, Gaudence Mmassy.
Kutokana na umuhimu wa utekelezaji wa diplomasia ya
uchumi ubalozi uliratibu jukwaa hilo hilo na kuendelea kuwahimizi wawekezaji
kuwekeza Tanzania kutokana na kuwa na mazingira wezeshi ya uwekezaji, maliasili
mbalimbali na sheria na sera rafiki, amani na utulivu.
Kutokana na Mkutano huo, kampuni zaidi ya 30
yameonesha utayari wa kuja nchini Tanzania kufanya ziara ya kibiashara na
kupata taarifa zaidi kwa ajili ya kufanya maamuzi ya uwekezaji.
Makampuni hayo yapo katika sekta ya afya, utalii,
ujenzi wa nyumba, viwanda, madini, mafuta, gesi asilia na Kilimo.