Katibu wa
Siasa, itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Shinyanga Bwana Richard
Masele akitoa taarifa kwa waandishi wa habari.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Shinyanga imemuachisha
nafasi ya uongozi Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) wilaya ya Shinyanga
Mjini Bwana Jonathan Agustino Madete kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Taarifa
hiyo imetolewa kwa waandishi wa habari na katibu wa Siasa, itikadi na Uenezi wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Shinyanga Bwana Richard Masele, ambaye amesema
maamuzi hayo yametolewa katika kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa
Shinyanga.
“Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM
Mkoa wa Shinyanga chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Mabala Mlolwa, kilichoketi
mnamo tarehe 13,06.2024, pamoja na mambo mengine kimemuachisha nafasi ya
uongozi ndugu Jonathani Agustino Madete Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Shinyanga
Mjini kwa sababu ya utovu wa nidhamu,”amesema Masele.
“Vilevile Halmashauri kuu ya CCM
Mkoa wa Shinyanga imeazimia kuwa, kwamwe haitamfumbia Macho wala kumvumilia Mtu
yeyote awe kiongozi au Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM, atakayevunja
kanuni,taratibu na Katiba ya Chama chetu, hatua za kinidhamu zitachukuliwa mara moja”.
“Hiini pamoja na kulinda heshima ya Chama chetu na Jumuiya zake na kuhakikisha misingi ya Chama hiki na miongozo inaendelea kuheshimiwa chini ya Mwenyekiti wetu mahiri, mchapa kazi na mzalendo wa kweli Mhe. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania”.amesema Masele
Katibu wa
Siasa, itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Shinyanga Bwana Richard
Masele akitoa taarifa ya kuvuliwa uongozi Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya
Shinyanga mjini Bwana Jonathan Madete.
TAZAMA VIDEO HII.