WAVUTIWA NA MIRADI YA MAENDELEO



WAZEE wa Kata ya Bujora wamefurahishwa na Miradi inayotekelezwa katika eneo hilo na kusema kuwa imekidhi viwango vya ubora unaotakiwa ambao umekuwa ukisisitizwa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mmoja wa wazee hao Mariam Shija alisema wamekoshwa na Utekelezaji wa Miradi katika Kata ya Bujora kwa kuwa katika ubora Mkubwa .

Mwananchi mwingine, Shaban Amon amepongeza kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassani na kutaka apitishwe bila kupingwa huku vilevile akibainisha Mbunge wao Deusdery Kiswaga kuwa katekeleza kwa vitendo ahadi alizotoa kwa Wananchi wake kwa kushirikiana na Diwani wa eneo hilo.

Vilevile Wananchi hao wameipongeza Kamati ya Siasa Wilayani hapo kwa kutambua kazi kubwa zilizofanywa na watendaji wake na kufanya sehemu hiyo kupendeza.







Previous Post Next Post