Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametoa wito kwa wananchi Mkoani
Shinyanga kuwa na utamaduni wa kupima Afya ili kufahamu hali ya Afya na namna
ya kujilinda na magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya kuambukiza.
Ameyasema hayo leo Jumanne Juni 18,2024 wakati akizungumza na wananchi waliojitokeza kupata
huduma bure ya Macho pamoja na huduma
zinazotolewa na madaktari bingwa wa Rais
Samia katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
RC Macha amesisitiza wananchi kujitokeza katika
huduma hizo huku akihimiza kuwa na utaratibu wa kupima Afya mara kwa mara
badala ya kusubiri kupatwa na ugonjwa.
“Ni
vizuri wananchi kujenga utamaduni wa kupima Afya zao wagonjwa wengi ambao
wanakuja Hospitali ni wagonjwa ambao pengine magonjwa yao yangeweza kuwa
yametibika au yameisha kabisa kama wangewahi kuja kupima yapo magonjwa kama
Saratani kwa upande wa akna Baba kuna matatizo ya tezi dume, kuna matatizo ya
figo, kuna matatizo ya mafuta kwenye miili yetu, kuna tatizo la Sukari haya
yote ni magonjwa ambayo kama tungeliweza kuwahi mapema katika Hospitali
tukafanya vipimo mfano ugonjwa wa Saratani ukiwahi mapema ukifahamika uvimbe
uvimbe kwenye maeneo yetu ya mwili ule ugonjwa unaisha kabisa, tumekubaliana na
nitakaa na viongozi wangu mganga mkuu na mamlaka zingine zote za Afya katika
Mkoa tutenge siku mbili kwa Mwezi ziwe ni mahususi kwa ajili ya watu kupima
Afya zao”.amesema RC Macha
Pia Mhe. Macha baada ya kutembelea ukarabati wa
majengo katika Hospitali hiyo amempongeza mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga
kwa usimamizi mzuri katika ujenzi na ukarabati wa majengo hayo.
“Lazima
niseme ukweli kwa sababu kuna nyakati tunafika mahali tunakemea kemea watendaji
lakini mali pengine ukifika ukawakuta watendaji wanafanya kazi vizuri unawasifu
kwakweli ni lazima tumsifu sana DMO wa hapa kazi anayoifanya kwa hakika
niyakuridhisha na tunaposema DMO lazima tuwashukuru na watumishi wa hapa kwa kazi
wanazofanya tunaona n kazi nzuri na tunazidi kuwatia moyo kuwahudumia wagonjwa
ni kazi kubwa sana kwahiyo inahitaji zaidi kwa wakati mwingine hata na utume
zaidi ya utumishi”.amesema RC Macha
Kwa upande wake mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga
Dkt. Elisha Robert ameeleza hatua
zilizofikiwa katika ukarabati na ujenzi wa majengo ya kutolea huduma ambapo
amesema ujenzi na ukarabati wa majengo hayo unagarimu zaidi ya bilioni moja.
“Tunatarajia
ifikapo Juni 30 ukarabati wa jengo la upasuaji utakuwa umekamilika pia zile
wodi mbili za wanaume na wanawake nazo zitakuwa zimekamilika lakini tunafanya
pia ukarabati wa jengo la kutunzia dawa tunaimani pia ifikapo tarehe 30 Mwezi
huu itakuwa imekamilika, maboresho yote ambayo tunayafanya ndani ya Hospitali
hii ya Manispaa ya Shinyanga ambayo yanajumuisha ujenzi pamoja na ukarabati wa
miundombinu ikiwemo ujenzi wa jengo la dharura, ujenzi wa jengo la OPD,
ukarabati wa jengo la upasuaji, wodi mbili za wazazi, jengo la kutunzia dawa,
jengo la mionzi pamoja na ukarabati mdogo wa jengo la maabara, CTC na TB clinic
utagharibu shilingi bilioni 1.3 fedha hizi tumeshazipokea kutoka kwa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan”.amesema
Dkt. Elisha
Katika taarifa ya uboreshaji miundombinu ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga iliyosomwa na kaimu Daktari mfawidhi Dkt.
Moshi Lyoba pamoja na mambo mengine amesema Hospitali hiyo inachangamoto ya
upungufu wa watumishi, vifaa tiba pamoja na uchakavu wa miundombinu.
“Manispaa
ya Shinyanga ilipokea huduma za Afya zilizokuwa zinatolewa na Hospitali ya
rufaa ya Mkoa wa Shinyanga hii ni kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa Hospitali
mpya ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo katika kata ya Mwawaza ambayo tayari
imeshaanza kutoa huduma za Afya upokeaji wa huduma za Afya kwenye Hospitali hii
ulifanyika kuanzia tarehe 01.07.2023”.
“Huduma
zinazoendelea kutolewa ndani ya Hospitali baaada ya kupokea ni huduma za wagonjwa
wan je (OPD), huduma za dharura (EMD), huduma za uzazi kwa Mama wajawazito
ikiwemo na upasuaji, huduma ya kulaza watoto, wanaume na wanawake, huduma za
kulaza watoto wachanga (NICU), huduma za maabara, huduma za mionzi (X-ray na
Ultrasound), huduma za tiba na matunzo (CTC), huduma za kifua kikuu, huduma za
kuhifadhi maiti, huduma za kinywa na meno na huduma kwa wagonjwa wa bima (NHIF
na Ichf)”.amesema Dkt. Lyoba
“Manispaa ya Shinyanga ilipokea fedha kiasi
cha shilingi 1, 300, 000,000\= kwa awamu mbili tofauti kwa ajili ya ujenzi na
ukarabati wa miundombinu ambapo awamu ya kwanza kiasi cha shilingi 500, 000,000\= kilipokelewa tarehe 04.01.2024 na kufuatiwa
na mapokezi ya shilingi 800,000,000\= katika awamu ya pili, kiasi hiki cha
fedha kilipokelewa kwenye akaunti ya Hospitali tarehe 26.02.2024 fedha hizi
zimelenga kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za Afya kwa kujenga jengo la
dharura, jengo jimpya la wagonjwa wa nje na njia za waenda kwa miguu (walk
way), kufanya ukarabati wa jengo la upasuaji, wodi mbili za upasuaji, jengo la
kutunzia dawa na jengo la mionzi pia kufanya ukarabati mdogo wa jengo la ICU,
Maabara, CTC na TB clinic”.
“Lengo
la mradi ni kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma za Afya kwa wakazi 214, 744
wa Manispaa ya Shinyanga na maeneo jirani, mradi huu wa uboreshaji wa
miundombinu ya kutolea huduma za Afya ndani ya Hospitali unatarajia kukamilika
ifikapo Juni 30, 2024”.
“Hadi
kufikia tarehe 18,06,2024 ujenzi na ukarabati huu ulikuwa umegharimu kiasi cha
shilingi 1,023,543,500\= hii ikiwa ni
gharama za vifaa vya ujenzi na ufundi ambazo zimelipwa kiasi cha shilingi
276,456,500 hazijatumika aidha vigae kwa ajili ya jengo la OPD vimenunuliwa
toka kiwandani”.amesema Dkt. Lyoba
Wakizungumza na Misalaba Media baadhi ya wananchi wa
Manispaa ya Shinyanga wametoa shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kupitia serikali yake ya awamu ya sita kwa
kuamua kuboresha mazingira ya kutolea huduma za Afya hali ambayo itasaidia
kuendelea kuimarisha Afya za wananchi.
Mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha
Robert akizungumza leo Juni 18,2024.
Mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha
Robert akizungumza leo Juni 18,2024.
Kaimu Daktari mfawidhi Dkt. Moshi Lyoba akisoma taarifa ya uboreshaji wa miundombinu ya Hospitali ya Manispaa ya
Shinyanga.
Kaimu Daktari mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya
Shinyanga Dkt. Moshi Lyoba akiwaongoza viongozi mbalimbali kutembelea ili kuona
namna wananchi wanavyopata huduma bora.
Mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha
Robert akimwongoza mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Mhe. Anamringi Macha pamoja na viongozi wengine katika kutembelea ujenzi na
ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika Hospitali ya Manispaa
ya Shinyanga.
Ziara ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi
Macha kutembelea na kukagua mradi wa uboreshaji miundombinu katika Hospitali ya
Manispaa ya Shinyanga ikiendelea leo Jumanne Juni 18,2024.
Mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akimwongoza mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha pamoja na viongozi wengine katika kutembelea ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Mganga mkuu wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elisha Robert akimwongoza mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha pamoja na viongozi wengine katika kutembelea ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Ziara ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi
Macha kutembelea na kukagua mradi wa uboreshaji miundombinu katika Hospitali ya
Manispaa ya Shinyanga ikiendelea leo Jumanne Juni 18,2024.
Mratibu wa elimu ya Afya kwa umma Manispaa ya
Shinyanga Salmon Mkanula akitoa elimu kwa wananchi ambao wamejitokeza kwa ajili
ya kupata huduma ya Macho katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga leo Juni
18,2024.
Post a Comment