Ziara ya vijana wa Mtoko wa Bata la kijanja
Shinyanga na Malula Tv imefanyikiwa ambapo wametembelea Miradi mbalimbali ya maendeleo
katika Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi wa Malula Tv, Bwana Daniesa Malula
amesema malengo ya ziara hiyo ni kuwaunganisha Vijana, kushare uzoefu,
kutatuliana changamoto kwa njia ya furaha na kuyasema na kuyaonyesha yale maendeleo
yote yaliyofanywa na serikali na viongozi wote wa Mkoa wa Shinyanga
Pia amesema ziara hiyo ni kuwatia moyo viongozi wote kwamba wanayoyafanya kwenye Mkoa wa Shinyanga yanaonekana
na kwamba mtoko huo ni sehemu ya kutambua na kuheshimu kazi zote zinazofanywa
na Mkuu wa Mkoa,Mkuu wa Wilaya, Mkurungezi, Mbunge pamoja na vijana kupitia
Program maarumu ya Mtoko wa bata la kijanja na Malula Tv.
Katika Mtoko huo wametembelea Bustani na maeneo la
kupumzikia watu hapa mjini Shinyanga, ambapo vijana hao wamesema Kalogo na
Stend ya Soko kuu wamevutiwa na kuihakikishia serikali ya awamu ya sita
kwamba inafanya kazi kwa vitendo katika
kuleta maendeleo kwa wananchi.
Mkurugenzi wa Malula Tv, Bwana Daniesa Malula
amesema ziara ya Mtoko wa vijana ni endelevu ambapo amewakaribisha vijana,
viongozi na wadau kuunga mkono ziara hizo huku akiwaomba wafadhili kujitokeza
kwa wingi.
Shinyanga yetu tuijenge pamoja “BATA LA KIJANJA NA
MALULA TV”