AFURAHIA SERIKALI KUFIKIA MAELEWANO NA WAFANYABIASHARA


MFANYABIASHARA Maarufu wa Dawa za binadamu (Pharmacy) Jijini Mwanza Malaki Mhoja ameipongeza Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia maombi ya wafanyabiashara juu ya ulipaji wa kodi.

Mkurugezi huyo wa Ifakara Pharmacy iliyopo katikati mwa Jiji la Mwanza alisema kitendo kilichofanywa na serikali kusikiliza kilio chao na kufanyia kazi ni hatua nzuri inayohitaji kuendelezwa Ili kuondoa changamoto kama hiyo kujirudia tena.

Alisema maridhiano baina ya wafanyabiashara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ni mhimu kufanywa kila wakati Ili kuwezesha mafanikio ya kiutendaji kazi hapa nchini kwani hali hiyo huepusha migogoro isiyo ya lazima.

"Naomba TRA iendelee kuzungumza na wafanyabiashara Ili kutatua changamoto zinazotukabili Ili tuweze kuwahudumia watanzania vizuri" alisema Malaki.

Wakati huohuo Mhoja ameiomba serikali kuendelea kuchochea wawekezaji wa Ndani na Nje kujitokeza na kuwekeza kwenye viwanda vya utengenezaji wa Dawa za binadamu Ili waweze kumudu kuwasambazia watanzania kwa bei ya chini.



Previous Post Next Post