Watu watatu wamepoteza maisha katika ajali ya Barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia jana Jumatatu Julai 1, katika Barabara ya Tinde –Kahama eneo la kijiji cha Puni kata ya Puni,Wilaya ya Shinyanga, Ikihusisha Bus la abiria la kampuni ya Abood kugongana na gari ndogo aina ya NOHA.
Akizungumza na Misalaba Media, Kaimu kamanda wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa polisi Kenedy Mgani amesema kufuatia ajali hiyo jumla
ya watu wanne wamejeruhiwa ambapo wawili
kati yao wamelazwa katika kituo cha Afya cha Bugisi na wengine wawili katika
hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo kata ya Mwawaza Manispaa ya
Sinyanga
Kaimu kamanda huyo amesema chanzo cha ajali hiyo ni
uzembe wa dereva wa gari ya NOA kuhama upande wake hivyo kugongana uso kwa uso
na Bus hilo la Abiria.