Watu watatu wameripotiwa kufariki na wengine nane kujeruhiwa baada ya kupata ajali katika kijiji cha Njirii Wilayani Manyoni Mkoani Singida, ajali iliyohusisha basi la kampuni ya Zube lililokuwa likitokea Mkoani Mwanza kwenda Dar es Salaam.
Ajali hiyo imedaiwa kuhusisha gari aina ya Eicher iliyokuwa imebeba chupa za soda ikitokea Itigi kwenda Singida na kusababisha kugongana uso kwa uso hadi kupelekea vifo vya watu watu watatu wakiwemo dereva wa basi na wa gari hiyo ya iliyobeba soda.
Juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP. Amon Kakwale ili kuzungumzia tukio hilo zinaendelea